Obama aapa kuangamiza Islamic State

Rais Obama ameahidi kuangamiza Wanamgambo wa Islamic State
Rais wa 
Marekani Barack Obama amesema Marekani itashambulia kundi linalojiitaa 
Islamic state kote nchini Syria na Iraq ili kuwanyima kabisa makao ya 
kujificha .
Bw Obama 
amesema kushiriki kwa mataifa kadhaa ya kiarabu katika mapambano hayo 
kunaonyesha wazi hivyo si vita vya Marekani pekee bali wao ni sehemu ya 
muungano wa mataifa yanayopigana na kundi hilo liitwalo pia ISIL.
Pia 
amekiri kuwa mashambulio hayo yamelenga pia wale aliowataja kuwa 
wanamgambo sugu wa al Qaeda wa kundi liitwalo Khorasan ambao anasema 
wanalenga kuishambulia Marekani.
Nazo taarifa za jeshi la Marekani zasema malengo ya mashambulio yaliyofanywa yametimia.BBC

Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa wakifanya mauaji na utekaji nyara
Wanamgambo kadhaa wa IS wameripotiwa kuuliwa japo vifo vya raia pia vimeripotiwa.
Mapema 
msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Alexander Lukashevichy 
amesema mashambulio yoyote dhidi ya ISIL ni sharti yazingatie sheria za 
kimataifa.
Kadhalika
 Obama, amesema kuwa kuhusika kwa nchi za kiarabu katika vita dhidi ya 
wanamgambo wa Islamic State nchini Syria ni dalili toshja kuwa vita hivi
 sio vya Marekani pekee.
Obama amesema ataendelea kukusanya jeshi la kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Saudi Arabia, Milki za kiarabu,Jordan na Bahrain zote zilituma ndege za kijeshiu katika opereshei hiyo
No comments:
Post a Comment