Hong Kong bado hali tete
Raia wa Hong Kong wakivurumushiwa moshi
Makumi
kwa mamia ya waandamanaji wa Hong Kong wanaendelea na maandamano yao kwa
siku nyingine tena baada ya kudhoofisha maeneo muhimu ya jiji hilo
wakati wa mchana. Waandamanaji hao sasa wanamtaka Mkuu wa utawala wa
Hong Kong Leung Chun-Ying ajiuzulu..
Wakati
huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong
na imeutaka utawala kuchukua hatua. Katika mkutano wa wanahabari
msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono
matakwa ya watu wa Hong Kong.
"Duniani
kote, na hii ni kweli katika Hong Kong na maeneo mengine, Marekani
inaunga mkono kimataifa, uhuru, kama vile uhuru wa kukutana kwa amani na
uhuru wa kujieleza. Marekani inautaka utawala wa Hong Kong kuchukua
hatua, na kwa upande wa waandamanaji kutoa maoni yao kwa amani"BBC
No comments:
Post a Comment