BENKI KUU YA TANZANIA IMETOA TOLEO JIPYA LA SARAFU YA SHILINGI 500

Sarafu ya shilingi 500 itakayoanza kutumika Oktoba 2014.
BENKI Kuu
 ya Tanzania imetoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500 itakayoanza 
kutumika Oktoba 2014 itakayokuwa mbadala wa Noti ya shilingi 500 
inayoonekana kuchakaa haraka.

Noti ya 500 inayotumika sasa.
Hayo 
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za kibenki wa
 benki hiyo Bw. Emmanuel Boaz wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Noti ya 
shilingi 500 hupita kwenye mikono ya watu wengi zidi na ndiyo 
inayotumika zaidi kwenye manunuzi ya kawaida hivyo kuchakaa haraka ndio 
maana tumeamua kutoa toleo la sarafu itakayoanza kutumika mapema mwezi 
wa 10 mwaka huu.”alisema Boaz.
Akifafanua
 zaidi Boaz amesema Sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa miaka mingi zaidi 
kuliko noti na pia noti zimekuwa zilikaa katika mzunguko kwa muda mrefu 
bila kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili zibadilishwe.(P.T)
        
Akitaja 
sifa za sarafu hiyo mpya Boaz amesema kwanza umbo lake ni la duara lenye
 michirizi pembezoni na kipenyo cha milimita 27.5 na uzito wa gramu 9.5.
Sifa 
nyingineni kuwa ina rangi ya fedha na imetengenezwa kwa madini aina ya 
chuma na Nickel na kwa upande wa mbele ina sura ya Rais wa kwanza wa 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume na kwa nyuma 
ina taswira ya mnyama nyati akiwa mbugani.
Pia Boaz 
alibainisha kuwa sarafu hiyo kwa upande wa nyuma ina kivuli 
kilichojificha ambacho huonesha thamani ya sarafu ya 500 au neno BOT 
inapogeuzwa geuzwa.
Kwa 
upande wa matumizi Boaz amesema sarafu hiyo itakapoanza kutumika 
itatumika sambamba na noti za shilingi 500 hadi zitakapokwisha kwenye 
mzunguko.
Benki Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la kutoa sarafu na noti halali (legal tender) zinazotumika nchini ambapo katika kutimiza jukumu hili Benki kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano mzuri wa thamani (denomination) unaozingatia uwezekano wa zile zenye thamani kubwa kuweza kugawika katika zile zenye thamani ndogo.
Benki Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la kutoa sarafu na noti halali (legal tender) zinazotumika nchini ambapo katika kutimiza jukumu hili Benki kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano mzuri wa thamani (denomination) unaozingatia uwezekano wa zile zenye thamani kubwa kuweza kugawika katika zile zenye thamani ndogo.
No comments:
Post a Comment