TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, September 23, 2014

RONALDO APIGA NNE REAL IKIUA 5-1 LA LIGA 

Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakishangilia ushindi wao wa 5-1 jana
NYOTA Cristiano Ronaldo amepiga hat-trick yake ya 25 akiwa na Real Madrid kikosi cha Carlo Ancelotti kikifikisha mabao 18 katika mechi tatu kufuatia ushindi wa 5-1 dhidi ya Elche katika La Liga.
Ronaldo alifikisha mabao nane ndani ya wiki na baada ya mechi alipoulizwa kama bado ana furaha Madrid alisema."Mambo yanakwenda vizuri na zaidi binafasi na timu inafunga mabao, inashinda mechi na kucheza vizuri.'(P.T)
Alipoulizwa kuhusu kauli ya karibuni ya Jose Mourinho kwamba wawili hao kwa sasa hawana uhusiano tena, "Si juu yangu kuzungumza mambo kama hayo, nafikiria juu ya kile tunachokifanya uwanjani," amesema.
Wageni walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Albacar Gallego kwa penalti ya utata iliyotolewa na refa Carlos Gomez, lakini Gareth Bale akasawazisha akimalizia krosi ya James Rodriguez kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga mabao manne, mawili ya penalti na kufikisha hat-trick 25 akiwa na Los Blancos.
Chanzo:bongostaz

No comments:

Post a Comment