TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, September 23, 2014

Risasi alizopigwa jamaa alietaka kumuua Mbunge kwa panga

short gun
Wakati Mbunge Steven Ngare akikagua mradi wa maendeleo kwenye shule ya msingi huko Kenya kuna jamaa alijitokeza na kujaribu kutaka kumvamia ili amkatekate kwa panga lakini kabla hajamfikia tayari mlinzi wa mbunge akawa amemuona.
Imetokea kwenye kijiji cha Kariti kaunti ya Kainyaga huko Kenya ambapo baada ya mlinzi kuona na kupata uhakika jamaa huyo alikua na nia mbaya, alichukua bastola yake na kumpiga risasi tatu zilizosababisha mwanaume huyo kufariki papohapo huku sababu zaidi za kwanini alitaka kufanya hivyo zikiwa hazijulikani.
Kwa mujibu wa Citizen TV, mtu huyu alitaka kumshambulia mbunge huyu muda mfupi tu baada ya kumkata kwa panga mwalimu mkuu wa shule hiyo kulikompa majeraha na kumfanya awe mahututi hospitalini hadi sasa.
NYINGINE
Taarifa nyingine kutoka Radio Jambo ya Kenya ni kuhusu hii ya mshukiwa mkuu wa mauaji ya Mbunge aitwae George ambae alifariki baada ya kunywa kinywaji kilichowekewa sumu, amepoteza kwa mara nyingine tena ombi la kutaka kuachiwa kwa dhamana kwa sababu alizozitoa kwamba ana matatizo ya kiafya.
Paul Wainaina ni mmiliki wa Baa ambako inadaiwa marehemu Mbunge George ndiko alikowekea sumu kwenye kinywaji chake.
NYINGINE:
Malipo ya umeme yatapungua nchini Kenya mwezi huu kutokana na kuanzishwa kwa miradi mingi zaidi ya kuzalisha umeme ambapo kampuni husika imesema huenda malipo hayo yakapungua kutoka shilingi 17 za Kenya mpaka shilingi sita kwa kilowati moja ambapo pia serikali ya nchi hiyo inajitahidi kufanikisha mradi wake wa kuongeza megawati elfu 5 za umeme kufikia mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment