ANAYEDAIWA KUWA TAPELI WA AJIRA ANASWA
Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
YAHAYA unaishi
wapi? Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter
amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya
Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.
Tapeli anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter.
Tukio
hilo lilitokea Septemba 19 mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Kimara
baada ya tapeli huyo kumlaghai dada mmoja aitwaye Wema Raymond wakutane
hapo kwa ajili ya vipimo vya ukimwi vilivyotakiwa kuambatanishwa katika
fomu ya kuomba nafasi ya kazi ambayo awali dada huyo alidai kupatiwa na
tapeli huyo.(P.T)
Akizungumza
na waandishi wetu, Wema alisema alimfahamu tapeli huyo kupitia kwa
rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Rebecca, ambaye naye awali alipigiwa
simu na mtu huyohuyo akimtaka kimapenzi.
Wema
alisema kuwa rafiki yake alimkatalia tapeli huyo, lakini siku chache
baadaye alimpigia tena akimwambia kulikuwa na nafasi ya kazi katika Chuo
cha Ardhi hivyo anamhitaji yeye kwa ajili ya nafasi hiyo.
“Kwa
sababu Rebecca ana kazi yake tayari aliamua kunitaarifu mimi kwa kuwa
anajua natafuta kazi,” alisema Wema.Alisema alikutana na jamaa huyo
ndani ya Chuo cha Ardhi na kupatiwa fomu aliyoelekezwa kujaza kisha
akatakiwa kutoa shilingi 280,000 kama malipo ya fomu hiyo na gharama za
mafunzo ya siku tatu ya vitendo kuhusu kazi, fedha ambazo hakuwa nazo
kwa muda huo na kulazimika kumuomba rafiki yake Rebecca amsaidie.
Wema Raymond aliyetapeliwa na tapeli huyo anayefahamika kwa jina la Baraka au 'Muba'.
“Baada ya
kumaliza mazungumzo pale chuoni akanisindikiza hadi nje, lakini cha
kushangaza pale mlangoni nikamuona anampatia mmoja wa walinzi hela,
nikamuuliza kwa nini aliwapa hela, akasema eti watu wengi wanaitaka
nafasi ile wakiwemo walinzi hao, hivyo alikuwa akiwapoza wasimsemee kwa
kunitafutia mimi kazi isije akafukuzwa kazi,” alisimulia Wema na
kuongeza kuwa alitakiwa kesho yake kupima VVU ili vipimo hivyo
viambatanishwe kwenye barua yake ya maombi.
Katika
Kituo cha Afya Kimara, alikutana tena na tapeli wake, aliyeonekana
kuwasalimia madaktari na manesi kana kwamba wanajuana kisha akaingia kwa
dokta na kuzungumza naye.Baada ya muda tapeli huyo alitoka nje kisha
akamwambie Wema aingie kwa daktari kwa ajili ya kujaziwa fomu hizo
kienyeji bila kupimwa maambukizi ya ukimwi.
“Nikiwa
ndani machale yalinicheza, ikibidi nimuulize yule daktari kama anajuana
na yule jamaa, daktari akasema kwamba hawafahamiani hata kidogo jambo
lililonishtua. “Nikamnong’oneza kuwa nahisi kutapeliwa, akaniambia
nikakae naye nikijifanya namuongelesha huku yeye akizunguka kwa mlango
wa nyuma na kuwaita mapolisi.
Kamanda Suleiman Kova.
“Katika
upekuzi alikutwa na zile pesa zangu za jana zikiwa kwenye simu yake na
shilingi 90,000 akiwa nazo mfukoni huku akionekana kutumia simu yenye
jina la Martha Peter ambalo mwenyewe alikiri kuwa alikuwa akinitapeli.”
“Polisi
walichukua maelezo yangu na kufungua jalada RB/4969/2014 KUJIPATIA PESA
KIUDANGANYIFU kisha wakaniambia nifike kesho yake,” alisema Wema na
kuongeza kuwa siku ya pili alipofika kituoni hapo aliwakuta watu wengine
waliodai kutapeliwa na jamaa huyo kwa majina tofauti na walipopiga
hesabu fedha alizowatapeli kwa pamoja zilifikia sh.1,435,000.
No comments:
Post a Comment