Mchinjaji wa IS atambuliwa

Mkurugenzi wa FBI James Comey
Mkurugenzi
 mkuu wa FBI James Comey amesema kitengo chake kimemtambua mtu ambaye 
huficha sura yake ambaye ni muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati 
akiwachinja mateka watatu kwenye video inayo nadi wanamgambo wa dola ya 
kiislam IS.
Pamoja na
 hayo Bwana Comey amegoma kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja jina
 lake,ingawa imeshajulikana lafudhi ya mtu huyo kuwa ni mwenye asili ya 
mji wa London, na Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu huyo 
umefanikishwa kwa msaada mkubwa wa marafiki wa kimataifa.
Muuaji 
huyo wa waandishi James Foley na Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa 
kujitolea David Haines walipigwa picha ya video na kuwekwa kwenye 
mitandao na wanamgambo hao wa dola ya kiislam na kusaidia kufanya 
maamuzi juu ya mipango ya wapiganaji wa jihad.BBC
No comments:
Post a Comment