TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, September 12, 2014

WAMA YAANDAA MKUTANO WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NA MATITI 

IMG_1907
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uragibishi (advocacy) kuhusu saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa akina mama kutoka katika nchi za Afrika Mashariki. Mkutano huo pia unahudhuriwa na wajumbe kutoka Zambia, Malawi, Madagascar na Zimbabwe. Katika picha wanaonekana wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa. Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika hoteli ya Courtyard  hapa Dar Es Salaam na umeandaliwa kwa pamoja kati ya WAMA na Shirika la WE CAN (Women Empowerment Cancer Advocacy Network) kutoka nchini Marekani.
IMG_1943
Washiriki wa mkutano wa saratani kwa akina mama wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi Dkt. William Kafura aliyemwakilisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii aliyefungua rasmi mkutano huo.
IMG_1946
Dkt. Williama Kafura akifungua rasmi mkutano wa uragibishi wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa akina mama katika nchi za Afrika Mashariki.
(Awadh Ibrahim)

No comments:

Post a Comment