RAIS KIKWETE HAWEZI KUAHIRISHA BUNGE
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha
Demokrasia Tanzania(TCD)Mhe. John Cheyo amesema kwamba mchakato mzima wa
Katiba utamalizwa kwa kura ya maoni ya wananchi, hivyo Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete haiwezi kutamka leo
kuliahirisha Bunge Maalum la Katiba kwa kuwa liko Kisheria.
Aidha
Mhe. Cheyo alisema kilichoahirishwa ni mchakato wa kura ya maoni ya
wananchi na si Bunge hilo kwa kuwa walikubaliana katika kikao cha
mashauriano, baina Rais Kikwete na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa
vyenye wabunge vinavyounda TCD kuwa bunge hilo liendelee.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bunge Mjini Dodoma na Mhe. Cheyo wakati wa mjadala
wa kujadili sura zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya, ambapo alisema
hayo ndiyo makubaliano yaliyofikiwa.
Aidha Mhe. Cheyo alisisitiza Katiba Mpya inayopendekezwa itakayopatikana itadumu kwa njia ya maridhiano.
“
Bunge hili linaendeshwa kwa mujibu wa sheria , Tangazo la Serikali
(Government Notice) Na 254 hili ndilo uhai wa Bunge hili hadi Oktoba 4,
mwaka 2014, na wote tukakubaliana haiwezekani Mhe. Rais akasema leo
Bunge likasitishwa.
“
Vitu viwili vikukutana kwa nia ya maridhiano, vitu vingine vinaweza
kuwekwa pembeni sawa na sasa na baadae vinaweza vinashughulikiwa kwa
wakati huo,” alisema Mhe. Cheyo.
Mhe.
Cheyo alisema anamwomba Rais Kikwete atoe ruhusa ya kuwepo kwa kipindi
maalum cha kitakachorushwa na televisheni (video) ili kila mtu
aonekana alichokisema, huku akionesha kusikitishwa na upotoshwaji wa
makubaliano hayo, uliofanywa na baadhi ya wanasiasa.
“
Mojawapo ambayo tuliyokubaliana Bunge hili lipate Katiba ambayo
inapendekezwa na wananchi pia kwa hali tulinayo haiwezekani mchakato
mzima ukamalizika, mchakato utamalizika kwa kura ya maoni ya wananchi.
Kama tukifika huko itabidi tuhairishe uchaguzi wa mwaka
2015. Niliyoyasema ndiyo makubaliano tuliyokubaliana,” alisisitiza.
Mhe. Cheyo alisema Rais Kikwete alikubali kukaa chini pamoja na TCD na hao wanaojiita Ukawa.
Alisema Rais
Kikwete alifanya mazungumzo na viongozi wa Vyama vya Siasa vyenye
wabunge vinavyounda TCD mara kwa mara ya kwanza, Agosti 31, mwaka 2014
kwa saa nne na mara ya pili, Septemba 8, mwaka 2014 kwa saa mbili.
Kikao
hicho cha mashauriano kilihusisha kamati ya makatibu wakuu, kamati ya
wenyeviti wa vyama vya CCM, CHADEMA,CUF na NCCR- Mageuzi.
(Awadh Ibrahim)
No comments:
Post a Comment