TAMISEMI YATAKA KUONGEZA ZAIDI KIWANGO CHA TAHADHARI YA UGONJWA WA EBOLA.
 Mganga
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Godfrey Mtei akipokea zawadi ya saa ya 
ukutani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, juzi mjini hapa.
 picha ya pamoja .
 Picha ya pamoja baadhi ya waganga wakuu wa wilaya na mikoa wakiwa na Mgeni rasmi , Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia.
 Waziri
 wa Tamisemi, Hawa Ghasia akikambishi zawadi ya saa ya ukutani Mganga 
Mkuu wa Serikali,Dk Donan Mmbando,saa hiyo iliyolewa na Taasisi ya Lab 
Eguip Limited.
 Baadhi
 ya waganga wakuu wa wilaya na Mikoa ya Tanzania Bara wakisiliza hotuba 
ya Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia ( hayupo pichani).
 Dk Frida Mokiti ( kushoto) akibadilishana mawazo na mwezake wakati wa mapumziko
Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, akiwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando , baada ya waziri kufungua mkutano.
Na John Nditi, Morogoro
WAZIRI
 wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 
(TAMISEMI),Hawa Ghasia, amewaagiza  Waganga Wakuu wa Mikoa , na 
Halmashauri za wilaya nchini kuongeza zaidi kiwango cha kuchukua 
tahadhari katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa Ebola.
Waziri
 Ghasia alitoa agizo hilo jana mjini hapa wakati wa  hotuba yake ya 
ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Waganga wakuu wa mikoa, Halmashauri za 
wilaya na wakurugenzi wa Hospitali za rufaa kutoka mikoa yote ya 
Tanzania bara.
Kwa
 mujibu wa Waziri huyo kuwa, hapa nchini ugonjwa huo  haujathibitika 
kuingia na Serikali imechukua tahadhari zote kuhakikisha kuwa ugonjwa 
huo hauingii  nchini na endapo utathibikika kuingia uweze kudhibitiwa 
kikamilifu.
Hata
 hivyo alisema , mwaka huu kumekuwepo na matukio ya hapa nchini na nje 
ya nchi yaliyotufanya tuongeze zaidi kiwango cha tahadhari , na tukio la
 kwanza ni la mlipuko wa ugonjwa wa Dengue , ambao uliwapata wagonjwa 
1,384 kote nchini, na kusababisha vifo vya watu wanne , sehemu kubwa ya 
wagonjwa walikuwa ni wa Dar es Salaam.
Kwa
 mujibu wa Waziri huyo , tukio la pili ni la ugonjwa wa ebola ,ambao 
kwanza ulianzia nchi za Afrika Magharibi,  na kati ya Machi hadi Agosti 
mwaka huu , watu 3,069 waliungua ugonjwa huo.
Hivyo  hadi
 kufikia Agosti 28, mwaka huu ,ugonjwa huo umeua watu 1,552 na hivi 
karibuni umeingia nchi ya Congo DRC na kufikia mwishoni mwa mwezi 
uliopita watu 24 wameripitiwa kuugua .
“
 Ni matumaini yangu kuwa katika mkutano huu  , suala la magonjwa ya 
mlipuko kama haya yatajadilikwa kikamilifu ili kila mmoja wenu awe 
katika tahadhari kubwa” alisisitiza Waziri Ghasia
Hata
 hivyo , Waziri Ghasia alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za Serikali ya
 Tanzania kwa Watu wa Marekani kupitia Shirika lao la CDC na Shirika la 
Afya Duniani kwa kutoa vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya kuzuia 
maambukizi ya ugonjwa huo wa ebola.
Mbali
 na tahadhari ya magonjwa ya mlipuko, Waziri Ghasia alisema , katika 
ziara zake sehemu mbalimbali hapa nchini ameshuhudia juhudi zinazofanywa
 na wadau katika kuboresha upatikanaji  na utoaji wa huduma za afya na 
ustawi wa jamii.
Kwa
 mujibu wa Waziri huyo kuwa juhudi hizo ni  kujenga vituo vipya vya 
huduma za afya , kukarabatiwa vituo ambavyo havipo katika hali 
nzuri  kuongeza watumishi na upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na 
kuimalisha utaratibu wa kukusanya mapato katika vituo.
Pia
 ulimalishaji wa utoaji wa huduma kwa makundi maalumu hususan , wanawake
 wajawazito, watoto chini ya miaka mitano na  wazee  katika baadhi ya 
maeneo husika.
Hata
 hivyo alisema ,kutokana na juhudi hizo, malalamiko kuhusu uhaba wa dawa
 na vitendo vya rushwa yamepungua katika maeneo ambako juhudi hizo 
zimekwishafanyika.
“
 Nimefurahishwa  na kasi ya ujenzi mpya wa Zahanati na Vituo vya Afya 
.... juhudi hizi zinapaswa kupongezwa  kwa vile ni utekeleaji wa Mpango 
wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)” alisema Waziri Ghasia .
Kwa
 upande wake Mganga Mkuu wa Serikali , Dk Donan Mmbando, kabla ya 
kumkaribisha waziri , alisema lengo la mkutano huo ni kujadili masuala 
muhimu yanayolenga kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii hapa 
nchini na pia kuainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi 
wa wizara hiyo.
Hata
 hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wataalamu hao wa sekta ya afya 
kujipanga kukabiliana magonjwa ya mlipuko ukiwemo wa ebola na kutenga 
maeneo maalumu kwa ajili ya kutolea huduma endapo kutakuwa na 
udhibitisho wa dalili za wagonjwa katika maeneo yao.
Pamoja
 na kuzungumzia changamoto zilizopo ikiwemo ya ya  usimamizi wa utendaji
 bora na uboreshaji wa  mazingira ya kazi na y a watumishi , pia 
aliwataka wataalamu wao kuangalia namna ya kukabiliana na ongezeko la 
magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo wa saratani.
Kwa
 mujibu wa Manga Mkuu wa Serikali, kuwa vituo vingi vya Afya vilijengwa 
kwa kuangalia upande mmoja wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na 
kusahau mengine yasiyoambukizwa na kwamba hatua zaidi zinapaswa 
kuchukuliwa ili kukabiliana nayo na kutaka yaingizwe kwenye mpango kazi 
wa mwaka 2016
No comments:
Post a Comment