CHARLES BONIFACE MKWASA ‘MASTER’ AULA TFF
Charles Boniface Mkwasa
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA
kocha wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa ameteuliwa kuwa Ofisa
Mtaalamu wa Elimu ya Mafunzo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa ameithibitishia BIN ZUBEIRY kwamba Mkwasa amepewa nafasi hiyo baada ya kurejea kutoka Uarabuni, alipokwenda kufundisha klabu.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa ameithibitishia BIN ZUBEIRY kwamba Mkwasa amepewa nafasi hiyo baada ya kurejea kutoka Uarabuni, alipokwenda kufundisha klabu.
Kwa
upande wake, Mkwasa, maarufu kama Master kwa jina la utani tangu enzi
zake anacheza nafasi ya kiungo Yanga SC na Taifa Stars, amesema kwamba
amekwishaanza kazi yake hiyo mpya TFF na anatarajia kuifanya kwa ufanisi
kwa sababu ana utaalamu nayo.(P.T)
Kuhusu
Mkataba wake na Yanga SC, Mkwasa alisema kwamba wakati anakwenda
Uarabuni alipewa likizo ya mwaka mmoja, lakini kwa sababu amerudi kabla
ya muda huo ameona bora kukubali kazi hiyo ya TFF kuliko kukaa bure.
"Kama
Yanga SC watanihitaji kurudi kazini kabla ya muda huo, ni suala la
kuzungumzika tu, kwa sababu TFF ipo kwa ajili ya maendeleo ya soka hapa
nchini na Yanga ni klabu ya Tanzania,"amesema mume huyo wa Mkuu wa
Wilaya ya Bahi, Dodoma, Betty Mkwasa, mtangazaji maarufu wa zamani wa
Redio na Televisheni.
Mkwasa
alijiunga na Yanga SC Desemba mwaka jana akitokea Ruvu Shooting ya
Pwani, lakini baada ya msimu Mei mwaka huu akaondoka pamoja na aliyekuwa
kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi Hans va der Pluijm kwenda Uarabuni.
Hata
hivyo, baada ya muda mfupi wa kufanya kazi huko, Pluijm aliyemchukua
Mkwasa kwenda naye huko- akatofautiana na uongozi wa timu na kusitishiwa
mikataba.
Wakati Pluijm alirejea Ghana anakoishi, Mkwasa alirudi nyumbani Tanzania na sasa anaibukia TFF..
Wakati Pluijm alirejea Ghana anakoishi, Mkwasa alirudi nyumbani Tanzania na sasa anaibukia TFF..
Chanzo:bongostaz
No comments:
Post a Comment