Ripoti yafichua udhalilishaji wanawake
Kikosi cha AMISOM, Somalia
Shirika
la haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti kuhusu
udhalilishwaji kijinsia wanaofanyiwa wanawake nchini Somalia na askari
wa kulinda amani nchini humo.
Majeshi
hayo yamo nchini Somalia yakiwakilisha Umoja wa Afrika na Umoja wa
Mataifa kupambana na wapiganaji wa kikundi cha Kiislam cha Al Shaabab.
Shirika
hilo la kutetea haki za binadamula Human Rights Watch limesema
liliwahoji wanawake 21, wakiwemo wasichana waliobakwa na wanajeshi hao
mwaka 2013.
Visa vingi vimeripotiwa katika kambi zinazosimamiwa na wanajeshi wa Burundi na Uganda.
Walinda
amani wa Muungano wa Afrika wamedaiwa katika ripoti hiyo, kutumia
chakula cha misaada kushawishi wasichana na wanawake kufanya mapenzi
nao.
Wanajeshi
hao wanadaiwa pia kuwabaka ama kuwadhalilisha kingono wanawake
waliofika katika kambi hizo kuomba msaada wa matibabu au maji.BBC
No comments:
Post a Comment