KIVUKO CHA MV. KIGAMBONI KUANZA KAZI KESHO KUTWA
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watendaji
mbalimbali hawapo pichani kutoka, Wizara ya Ujenzi, TEMESA na Kikosi cha
Maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamefanya kazi
kubwa ya ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ngazi kwenda
kukagua Kivuko cha MV Kigamboni ambacho matengenezo yake makubwa
yanakamilika leo.
Luteni
Kanali Gwanafi kulia akimuongoza Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli kwenda kukagua Kivuko cha MV Kigamboni sehemu ya chini
mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.
Luteni Kanali Gwanafi wapili kutoka kulia akitoa maelezo kuhusu ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Kigamboni kama inavyoonekana.
Taswira-Kivuko cha MV Kigamboni kinavyoonekana mara baada ya Ukarabati wake.
Luteni
Kanali Gwanafi kulia akimuonesha Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli sehemu ya juu ya Kivuko cha MV Kigamboni.
Luteni
Kanali Gwanafi kushoto akimuonyesha Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu
sehemu ya chini ilivyokarabatiwa.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha
MV Kigamboni huku akipatiwa maelezo kuhusu ukarabati wake.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini
Luteni Kanali Gwanafi kuhusu mambo mbalimbali wanayofanya ndani ya
kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka ndani ya Kivuko
cha MV Kigamboni mara baada ya ukaguzi wake. Picha zote kwa Hisani ya
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa
Kivuko cha MV Kigamboni kinatarajiwa kuanza safari zake za
usafirishaji rasmi kesho kutwa mara baada ya ukarabati wake
kukamilika.
Waziri wa Magufuli alitoa kauli hio leo wakati akikagua kivuko
hicho ambacho kilikuwa kikikarabatiwa na Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) kupitia kikosi cha Wanamaji.
Mheshimiwa Magufuli aliongeza kuwa hicho ambacho
kinategemewa na wananchi wengi waishio Kigamboni na maeneo
jirani kinategemewa kuteremshwa majini kesho jioni mara baada
ya maji kujaa na kesho kutwa kuanza rasmi shughuli zake za
usafirishaji.
“Nimekagua na kujionea kazi inavyoendelea na nimeridhishwa na
mlipofikia mpaka sasa, naamini kazi imefanyika ipasavyo, hivyo
basi palipobaki ni matengenezo madogo, kutokana na utendaji
wenu wa kazi naamini kesho Kivuko hicho kitateremshwa majini
na kesho kutwa kuanza safari”, Alisema Waziri Magufuli.
Aidha, Mheshimiwa Magufuli alikipongeza kikosi hicho cha
Navy kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa
wanamaliza ukarabati huo kwa wakati licha ya changamoto nyingi
walizokumbana nazo.
Sambamba na hilo, Waziri Magufuli amesema kuwa ndani ya Wiki
tatu au nne Boti ya Kutoka Dar hadi Bagamoyo itawasili kwani
imeshateremshwa majini huko inapotengenezwa na kilichobaki ni
kuifikisha Dar es Salaam
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi
Mussa Iyombe, amepongeza Jeshi la Wananchi Tanzania
kupitia Kikosi cha majini kwa uzalendo wao waliouonesha kwa
kukamilisha ujenzi huo kwa gharama nafuu na kwa wakati ili
kurejesha huduma za usafirishaji.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA), Mhandisi Marceline Magessa amesema
kuwa ukarabati wa MV Kigamboni ulikuwa katika hatua za
marekebisho mbalimbali ikiwemo utoaji kutu, kupaka rangi, usafi
na uzibaji wa matundu pembezoni mwa kivuko hicho.
Naye kamanda wa kikosi cha majini Brigedia Jenerali Rogastian
Laswai amezitaja changamoto zilizowakabili wakati wa
utengenezaji wa kivuko hicho kuwa ni pamoja na kushindwa
kupaka rangi kutokana na uwepo wa mvua pamoja na kupwa na
kujaa kwa maji
Ukarabati wa Kivuko cha MV Agosti 14 mwaka huu mpaka
kukamilika kwake hivi leo.
No comments:
Post a Comment