LIVERPOOL YABANWA 2-2, YATOKEA KWENYE PENALTI 14-13 ANFIELD
Mario Balotelli akipambana jana Anfield
KLABU ya
Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya
Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2
ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield.
Kinda
Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya
kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia
wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter.
Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa zimefungana 1-1 baada ya dakika 90.(P.T)
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi wao jana
Suso
akafunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool kuwapatia bao la
kuongoza Wekundu hao, lakini Kolo Toure akacheza rafu ndani ya boksi na
Patrick Bamford akaenda kusawazisha dakika za lala salama na katika
penalty Liverpool ikashinda 14-13 baada ya Albert Adomah kupoteza mkwaju
wa Boro.
Kikosi
cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Toure, Sakho, Enrique,
Rossiter/Williams dk79, Lucas, Sterling, Lallana, Markovic na
Lambert/Balotelli dk74.
Middlesbrough; Blackman, Fredericks, Ayala, Omeru, Friend, Adomah, Clayton, Leadbitter, Reach, Tomlin na Kike/Wildschut dk76.
Chanzo:bongostaz
No comments:
Post a Comment