JK ATAKA MSAADA ESRF KUONDOA UMASKINI KWENYE UCHUMI UNAOKUA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Hoseana Lunogelo akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini , Alvaro Rodriguez nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya mgeni
rasmi kuwasili kwenye mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia
ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa
jamii uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency,
Kilimanjaro.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi wetu
RAIS
Jakaya Kikwete amewataka nguli wa masuala ya uchumi na maendeleo ya
binadamu kuisaidia serikali kufanikisha azma yake ya maendeleo kwa
wananchi hasa ikizingatiwa kwamba zipo raslimali za kutosha, uchumi
unakua lakini umaskini haupungui.
Rais
alisema hayo jana wakati akifungua mkutano mkubwa wa tatu wa Taasisi
Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) unaozungumzia ukuaji wa uchumi
kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii uliofanyika
hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
Katika
hotuba yake kwa wataalamu nguli hao ambao wanaangalia athari za kisera
na kutoa ushauri katika masuala ya maendeleo yenye kulenga kunufaisha
jamii, alisema katika miaka 10 iliyopita uchumi wetu umekua ukikua kwa
kasi lakini hali hiyo haikuweza kusaidia kupunguza umaskini kama
ulivyolengwa na serikali...(MC)
Alisema
moja ya malengo ya millennia yalikuwa ifikapo mwaka wa kesho hali ya
umaskini ipunguzwe angalua nusu yake, kwa kuongeza pato la mtu binafsi
lakini hali sivyo ilivyo.
Rais
ambaye alitumia muda mwingi kueleza maendeleo ya kiuchumi yaliyofikiwa
katika hatua ya kuifikisha nchi hii miongoni mwa mataifa yenye kipato
cha kati ifikapo mwaka 2025, alisema zinatakiwa juhudi kubwa ili kuondoa
umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo (kushoto) akiteta jambo na Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez nje ya
ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
“Pamoja
na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ustawi wa jamii kama
uandikishaji wa watoto shule, uzazi na upunguzaji wa vifo vya watoto,
taifa bado linakabiliwa na changamoto kubwa ya ubora wa elimu,
upunguzaji wa vifo kwa wanawake wazazi na utapiamlo” alisema Rais
Kikwete.
Alisema
kwa kuangalia takwimu hizo katika jamii na ukuaji wa uchumi ni dhahiri
kwamba taifa letu ili kufikia malengo yake kuna mambo mengi yanatakiwa
kufanyiwa kazi na kuamini kwamba wataalamu hao katika mada zao
mbalimbali watakazojadiliana watatoka na kitu cha maana kuisaidia
serikali kupata mwelekeo sahihi wa kufikia taifa lenye kipato cha kati
ifikapo mwaka 2025.
Dira
ya maendeleo ya mwaka 2025 ambayo inayotaka kuifanya Tanzania kuwa nchi
ya kipato cha kati yenye maisha bora, utawala bora na uchumi wenye
ushindani miongoni mwa mambo machache yenye upeo wa juu yaliyomo katika
dira hiyo ndiyo yanayotumika kujadili na hatimaye kuipa serikali
majawabu ya mambo muhimu yanayotikisa safari ya kuelekea huko.
Ili
kufika huko kwa mujibu wa Rais Kikwete viashiria kadhaa vitaonekana
ikiwa ni pamoja na kushuka kwa mchango wa kilimo kwa pato la taifa na
ajira, kukua kwa sekta ya kisasa ya viwanda na huduma kwa uchumi, kukua
kwa miji na mabadiliko katika vizazi na vifo ambapo taifa linaondoka
katika vifo na uzazi wa fujo na kuwa na vizazi vidogo na vifo kidogo
kutokana na kukua kwa elimu na huduma za afya.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF Dk. Hoseana Lunogelo (kushoto) akiongozana na Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez kuelekea
kwenye ukumbi wa mkutano.
Alisema
mpango wa muda mrefu umelenga ifikapo mwaka 2025 mchango wa kilimo kwa
pato la taifa utapungua kutoka asilimia 27.8 kufikia 20.7, mchango wa
viwanda kupanda kutoka 24.4 hadi 30.7 na mchango wa huduma utapanda
kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2010 hadi 48.6.
“Ni
matumaini yangu kwamba wastani wa idadi ya watu ikipungua kutokana na
elimu na huduma safi za afya au ukuaji wa kasi wa pato la taifa kuliko
ongezeko la watu na hivyo kipato kitaongezeka na umaskini utapungua”
Miaka 10 iliyopita mchango wa kilimo katika pato la taifa umekuwa mkubwa huku vizazi na vifo vikiwa ni vingi.
Mkutano
huo ambao unajadili mabadiliko ya kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya
jamii unatokana na ripoti ya mradi wa maendeleo ya jamii (THDR)
iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Wageni waalikwa wakipitia ripoti mbalimbali zilizoandaliwa na ESRF nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi.
Naye
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez
akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa katika mkutano huo amesema
Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Tanzania kutengeneza ustawi kwa
wananchi wake.
Alisema
pamoja na kuwapongeza ESRF kwa kuandaa mkutano huo muhimu wa kuipatia
serikali fikira za namna ya kuboresha hali za wananchi wake.
Alisema
amefurahishwa kwa ESRF kusaidia kutafuta mustakabali wa maendeleo kwa
minajili ya kuendeleza wananchi kwani maendeleo ya kweli ni yale
yanayoboresha maisha ya wananchi.
Aidha
alivitaja vigezo muhimu vya maendeleo ya jamii katika hali ya uchumi
unaokua ambavyo ni kuhakikisha kwamba kuna usawa katika ukuaji wa uchumi
na maisha ya wananchi, kuongeza uwezo wa kuhami maendeleo yaliyofikiwa
dhidi ya haki zisizotabirika zinazovuruga ustawi,Kuhakikisha maendeleo
endelevu ya wananchi na nchi na kuendelea kuwasaidia wanaume kwa
wanawake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo iwe kiuchumi,
kijamii na kisiasa na kugawana kwa usawa matunda ya maendeleo.
Mratibu
wa Programu kutoka ESRF, Yasser Manu (kulia) akibadilishana mawazo na
baadhi ya wafanyakazi wenzake nje ya ukumbi wa mikutano kabla ya
kuwasili kwa mgeni rasmi.
Amesema
Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwamba
amefurahishwa na taarifa kwamba mkutano huo utajadili mada mbalimbali na
kutolea ushauri kwa kuzingatia taarifa ya THDR.
Awali
akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF Philemon Luhanjo, kumkaribisha
rais Jakaya Kikwete Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Hoseana Lunogelo
alisema wakati taasisi hiyo inaadhimisha miaka 20 ya uwepo wake, katika
mkutano wake wa 3 wa kitaifa wanatarajia wanazuoni kuchambua mada
mbalimbali na kuandika kitu kitakachosaidia serikali katika kuhakikisha
maendeleo ya kiuchumi yanakwenda sanjari na ustawi wa jamii kwa maana ya
kuondokana na umaskini katika ngazi ya mtu mmoja mmoja.
Mada zinazochambuliwa zinatoka kwa wataalamu waliobobea kutoka Tanzania,Ethiopia, Uingereza, Norway na India.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo akibadilishana mawazo na Balozi
wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada wakati wakimsubiri mgeni rasmi
kuwasili ukumbini hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo mara baada ya
kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro kufungua mkutano
mkubwa wa tatu wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF)
unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo
yanayogusa jamii.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo (kushoto) akiongozana na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)
pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo (katikati)
kuelekea ukumbi wa mikutano.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili ukumbini kufungua mkutano mkubwa wa tatu wa Taasisi Huru ya
Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa
kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii. Katikati ni
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Meza
kuu, Katikati ni mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha,
Prof. Adolf Mkenda, Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez ( wapili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya ESRF, Philemon
Luhanjo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo
(wa pili kushoto).
Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo akisoma taarifa ya taasisi yake
mbele ya mgeni rasmi wakati wa mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF
unaozungumzia ukuaji wa uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo
yanayogusa jamii sambamba na kutimiza miaka 20 ya tasisi hiyo tangu
kuanzishwa kwake uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt
Regency, Kilimanjaro.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa
mkono wa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo
mara baada ya kusikiliza taarifa ya maendeleo ya ESRF.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ESRF Philemon Luhanjo, akizungumza neno fupi kabla ya
kumrabisha mgeni rasmi Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kufungua rasmi mkutano huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akifungua rasmi mkutano mkubwa wa tatu wa ESRF unaozungumzia ukuaji wa
uchumi kwa kutumia fursa zilizopo na maendeleo yanayogusa jamii
uliofanyika jana jijini Dar katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro.
Mkurugenzi
wa Programu wa ESRF ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa taarifa ya
maendeleo ya watu nchini Tanzania (THDR), Dr. Tausi Kida akifuatilia kwa
makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Prof. Sylvia Temu akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano huo. Kulia
ni Gelase Mutahaba kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kushoto ni Prof.
Bertil Tungodden kutoka nchini Norway na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini
ESRF, Prof. Sylvia Temu (wa pili kushoto).
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini, mabalozi, taasisi mbalimbali za serikali waliohudhuria mkutano
huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar.
Kwa picha zaidi MOblog.....(MC)
No comments:
Post a Comment