MBUNGE KESSY ASIPIGWE, AJIBIWE HOJA ZAKE
Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kessy akisisitiza jambo.
Mbunge wa
Nkasi (CCM), Ally Kessy wiki iliyopita alilazimika kusindikizwa na
askari wa Bunge la Jamhuri kuondoka katika viwanja vya eneo hilo
kumnusuru na hasira za wajumbe kutoka Zanzibar waliokerwa na mchango
wake kuhusu masuala ya Muungano.
Kessy
alisimama bungeni hapo kutoa mchango wake kuhusu Katiba ya Jamhuri
akijikita zaidi katika suala la muundo wa Muungano na kusema kwamba
Zanzibar inabebwa na Tanganyika.
Nimnukuu,
alisema: “Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanganyika inabeba mzigo mkubwa ambao
haubebeki, hapa tunahudumia wabunge 83 kutoka Zanzibar ambao wanatibiwa
wao na wake zao na watoto kwa gharama za Tanganyika wakati hawachangii.”
Aliongeza
kuwa haiwezekani kwa Tanganyika kubeba mzigo mkubwa kama huo wakati
katika Jimbo lake la Nkasi wananchi wanalia na shida ya maji.Alisema
katika kamati yao Namba Moja, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu
alitoa semina iliyoonyesha kuwa Zanzibar haichangii chochote kwenye
Serikali ya Muungano na kuwa hata mishahara wakati mwingine wanategemea
Tanganyika.
Kessy
alisema wananchi wakilijua jambo hilo, wataikataa katiba inayopendekezwa
na kuitupilia mbali kwa kuwa inatoa upendeleo kwa Wazanzibari na
kuikandamiza Tanganyika.GPL (P.T)
“Mimi
naweza kuwa na wanawake sita, nikazaa nao lakini kila mtoto anaendelea
kutunzwa na baba yangu, jambo kama hili halivumiliki hata kidogo japo
najua kuwa ukweli unawauma,” alisema huku baadhi ya wajumbe wakipaza
sauti wengine kumpinga na wengine kuomba mwongozo wa mwenyekiti.
Lakini
ninachotaka kusema hapa ni kwamba wananchi wengi wa Tanganyika
niliozungumza nao katika utafiti wangu usio rasmi wanaungana na mbunge
huyo.
Hapa Dar
es Salaam baadhi ya wakazi wanasema iweje Zanzibar yenye watu milioni
moja na ushee wawe na wabunge 83 wakati jiji lao lina wakazi zaidi ya
milioni nne na lina wabunge wasiozidi kumi?
Alipinga
suala la Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa Muungano kwa maelezo
kuwa katika mfumo wa vyama vingi jambo kama hilo haliwezekani na kuhoji
itakuwaje awe makamu wa kwanza wa rais wakati hajachaguliwa na wananchi
wa Tanzania Bara?
Baada ya
kauli hiyo, kelele za wajumbe kutoka Zanzibar ziliongezeka baadhi
wakisimama na kuwasha vipaza sauti kumshambulia Kessy hivi: “Chizi huyo,
chizi huyo, hafai kwanza ni Mwarabu,” zilisikika sauti huku nyingine
zikimtaka aombe radhi.
Ukweli ni
kwamba alichokizungumza Kessy ndizo kero za muungano kwa upande wa
Tanganyika. Kati ya watu 50 niliowauliza jijini Dar kuhusiana na kauli
hizo, ni wawili tu waliopingana naye, hivyo ni dhahiri kwamba kauli yake
inapaswa kutazamwa.
Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kwamba wachache wakitokea
na kutoa wazo ambalo baadaye linaweza kuleta vurugu, ni bora
likakubaliwa kama halina madhara. Hivyo hayo ya Kessy yatazamwe na
yasipelekwe kisiasa.
Sikuona
sababu za wajumbe kutoka Zanzibar kumshambulia Kessy wakati aliyesema
hayo ni Gavana wa Benki Kuu, Bwana Ndulu yeye alikuwa akirudia na ndiyo
maana akasema hayupo tayari kuomba radhi.
Alidai
Ndulu alikuja katika kamati na akasema kwamba tangu kifo cha Abeid
Karume (rais wa kwanza wa Zanzibar), Zanzibar hawajawahi kuchangia
muungano, hili lilikuwa ndilo la msingi la kulijadili kama ni kweli au
ni uzushi na siyo kuzomea na kutaka kumpiga mtoa hoja.
No comments:
Post a Comment