TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, January 30, 2014

WAZIRI NYALANDU AAGIZA WAVAMIZI KUONDOKA

nyalandu_eb397.png
Na mwandishi wetu mwananchi
Tabora. Serikali imesema haitaogopa wala kumvumilia mtu atakayevamia maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba kwa lengo la kuhujumu maliasili.
Hali kadhalika kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika maeneo hayo.
Pia, imewataka watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi kuondoka kwa hiyari yao badala ya kusubiri kuondolewa kwa nguvu.
Hayo yalisemwa juzi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipokuwa akizungumza na maofisa na watumishi wa Idara ya Wanyamapori katika Kanda ya Magharibi.
Agizo hilo limetokana na taarifa za kuvamiwa kwa baadhi ya maeneo ya Hifadhi za Pori la Akiba la Ugalla na Moyowosi, ambapo baadhi ya wafugaji wameingiza mifugo huku baadhi wakijihusisha na ujangili.
Maofisa wa wanyamapori walisema wafugaji hao wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuingia na silaha kwenye hifadhi na kuwinda wanyama wakiwemo tembo na mamba.
.
Nyalandu alisema wavamizi wote wa hifadhi za taifa na mapori ya akiba wataondolewa kwa mujibu wa sheria.
''Nataka wale wote waliovamia mapori ya akiba na hifadhi za taifa waondoke kabla sheria haijachukua mkondo wake. Hakuna ruhusa ya kuingiza mifugo wala kuendesha kilimo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa, tutachukua hatua kwa hili,'' alisema.
Pia alisema Serikali imewataka watu wote wanaomiliki silaha zinazotumika katika ujangili kuzisalimisha ili wasichukuliwe hatua.
Waziri Nyalandu wakati umefika kwa kila Mtanzania kulinda rasilimali za nchi na kwamba wanaotaka kupora rasilimali hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Tutatumia nguvu zetu zote kuhakikisha kuwa tunalinda rasilimali zetu kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola nchini ili kumaliza ujangili nchini."
Alisema si ujangili wa kuua wanyama pekee unaoathiri nchi bali hata wafugajji wanaoingiza mifugo katika hifadhi na kuharibu mazingira watachukuliwa hatua.

No comments:

Post a Comment