Jenerali wa Sudan Kusini auwawa Bor
Mmoja wa wanajeshi wa jeshi la Sudan Kusini.
Mapigano makali yamezuka nje ya mji mkuu wa Sudan Kusini wa Bor na Jenerali mmoja wa jeshi la Sudan Kusini ameuwawa.
Mwandishi wa BBC anasema vikosi vya
serikali vinazidi kuelekea karibu na mji wa Bor ambapo kumekuwa na
mapigano ya kutegeana baina ya majeshi ya serikali na vikosi vya waasi
vinavyomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
Mwandishi wetu amesema pia ameshuhudia miili ya watu ikiwa chini na vifaru vikiwa vimelipuliwa vibaya pembezoni mwa barabara.
Pande pinzani nchini humo zinataraji kuanza mazungumzo ya ana kwa ana mjini Adis Ababa kujaribu kumaliza wiki tatu za mapigano.
Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya
Sudan kusini Nial Deng Nial amesema kuwa ni muhimu kwamba viongozi
kuzungumzia kuhusu kusitishwa kwa vita.(P.T)
No comments:
Post a Comment