UPINZANI UKRAINE, WATOA ONYO KWA SERIKALI
Waandamanaji wakipambana na polisi mjini Kiev(MM)
Vifo hivyo ni vya kwanza tangu kuzuka
kwa maandamano ya kuipinga serikali miezi miwili iliyopita. Waandamanaji
na polisi nchini Ukraine wamepambana tena mapema leo (23.01.2014),
baada ya ghasia kuzuka hapo jana Jumatano na kuigeuza sehemu ya katikati
ya mji mkuu, Kiev kuwa uwanja wa vita, huku polisi wakitumia mabomu ya
kutoa machozi na risasi za mpira dhidi ya waandamanaji waliokuwa
wakirusha mawe.
Vifo hivyo vimezusha hofu mpya baada
ya miezi miwili ya maandamano ya kuipinga serikali yaliyochochewa na
hatua ya serikali kutosaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na
Umoja wa Ulaya, kutokana na shinikizo la Urusi.CHANZO DWSWAHILI
No comments:
Post a Comment