Familia ya soka yampoteza gwiji Eusebio
Eusebio kushoto enzi zake akiwa na Pele Mwaka 1966 katika mechi kati ya Ureno na Brazil.
Eusebio da Silva Ferreira
Gwiji wa soka kutoka taifa la Ureno, Eusebio amefariki dunia.
Alikuwa na miaka 71 na kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Eusebio alizaliwa nchini Msumbiji kama
Eusebio da Silva Ferreira na anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora
zaidi kuwahi kutokea duniani.
Aliitumikia klabu ya mjini
Lisbon,Benfica FC kwa miaka 22 ambapo uwezo wake wa mbio na kasi,
kuutumia vyema mguu wake wa kulia na mbinu za kimpira kulimpa umaarufu
sana nchini Ureno na kubatizwa jina la The Black Pearl or the Black
Panther.
Wakati wa uchezaji wake alifunga mabao
733 katika mechi 745, pia alifunga mabao tisa kwenye michuano ya kombe
la dunia ya mwaka 1966 na kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo na
kuisaidia Ureno kushika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.(P.T)
No comments:
Post a Comment