TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, January 28, 2014

ITF YAIBEBA TENISI YA TANZANIA

tenis1 e6a77
Shirikisho la Tenisi la Kimataifa (ITF) limetoa nafasi moja ya upendeleo kwa mchezaji wa Tanzania kushiriki kwenye mashindano ya Tenisi ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 18 yaliyopangwa kufanyika mapema Machi katika nchi mbili tofauti. (HM)
Awali Tanzania ilipitisha wachezaji wanne waliofuzu kushiriki kwenye mashindano hayo ambayo yatafanyika jijini Nairobi, Kenya kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 16 na Cassablanca, Morocco kwa wachezaji chini ya miaka 18.
Kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya vijana, Kiango Kipingu, chama cha Tenisi Tanzania (TTA) kimepewa nafasi nyingine moja kwenye michuano hiyo ambayo ITF imesema itachagua yenyewe mchezaji huyo ambaye itamghariamia kwa kila kitu.
"Kutokana na motisha hiyo ya ITF sasa Tanzania itawakilishwa na wachezaji watano ambao wanne kati yao walifikia viwango vya kushiriki mashindano ya Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye yale ya Afrika Mashariki na kati hivi karibuni jijini Dar es Salaam," alisema Kipingu.
Alisema wachezaji waliofikia viwango, watatu wako Nairobi ambako huko wameweka kambi na watashiriki kwenye mashindano ya dunia ya vijana chini ya miaka 18 yanayoendelea kwa wiki tatu jijini humo ambayo yatakuwa sehemu ya maandalizi yao.
"Tumaini Mishuko, Emmanuel Malya na Omary Sule wako Nairobi ambapo baada ya mashindano ya dunia watakwenda Morocco kule watashiriki mashindano mengine ambayo yatakuwa sehemu ya maandalizi yao," alisema.
Kiango alisema, Georgina Kaindoa ambaye pia amefuzu anaendelea na mazoezi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mashindano hayo ya Afrika na kuongeza kuwa wanategemea kuwagawa wachezaji hao baadhi kushiriki mashindano ya Cassablanca na wengine yale ya Nairobi. Chanzo: Mwananachi

No comments:

Post a Comment