SERIKALI YA SUDANI KUSINI NA WAASI WATIA SAINI MAKUBALIANO
Serikali ya Sudan Kusini na upinzani
wametia saini mikataba miwili alhamisi katika mji mkuu wa Ethiopia,
Addis Ababa. Mkataba wa kwanza ni sitisho la haraka la hatua za kijeshi
na wa pili unahusu kuachiliwa kwa wafungwa 11 wa kisiasa ambao wametiwa
ndani tangu kuanza kwa mzozo katikati ya mwezi Disemba mwaka uliopita.
Mazungumzo ya amani yameongozwa na
taasisi ya kieneo IGAD na yalianza mapema mwezi uliopita. Mpatanishi
mkuu wa IGAD, Seyoum Mesfin anasema hatua kadhaa zinahitaji kuchukuliwa
na pande zote kwa vile hivi sasa wametia saini mikataba miwili.(M.M).
Bwana Seyoum anasema moja ni kutekeleza mikataba ambayo wametia saini kwa nia nzuri na ya dhati. Pili, kuanza kufanya kazi za ukarabati na kuwasaidia maelfu ya watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi na wakimbizi. Tatu, lazima tuendelee haraka na majadiliano ya kisiasa na kufanya kazi kuelekea katika maridhiano ya kitaifa.
Mkataba wa sitisho la mapigano unayataka majeshi ya serikali na upinzani kubakia walipo. Wanajeshi wa Uganda ambao wanaisaidia serikali ya Sudan Kusini itawalazimu waache operesheni zote katika muda wa saa 24.
Mkataba unaozungumzia wafungwa 11 haujaelezea wataachiliwa lini.Hakuna maneno ya kirafiki yaliyozungumzwa kati ya serikali ya Sudan Kusini na upinzani wakati wa sherehe za utiaji saini.
Chanzo, voa.swahili.com
No comments:
Post a Comment