AU KUZUNGUMZIA MIGOGORO AFRIKA
Viongozi wa Afrika wameanza mkutano
wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambapo agenda yao kuu
itakuwa swala la mizozo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan
Kusini.
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa
tume ya Umoja huo Nkosazana-Dlamini Zuma amewaambia viongozi 54 ambao ni
wanachama wa Muungano wa Afrika, kwamba wanapaswa kushirikiana ili
kuleta suluhu ya kudumu kwa migogoro Afrika.
Jamhuri ya Afrika ya kati imekumbwa na mgogoro wa kisisa kwa miezi kumi sasa tangu waasi kuipindua serikali.
Katika taifa jirani ya Sudan Kusini, makundi hasimu yalitia saini ya mapatano juma lililopita baada ya mapigano makali yaliyodumu mwezi mmoja, lakini mapigano yangali yanatokota kati ya serikali na waasi.
Maelfu ya watu wameuwawa katika mzozo huo.
Mkutano huo pia utaangazia,tatizo la uhaba wa chakula na kilimo katika bara hilo. Licha ya uchumi kukuwa katika sehemu nyingi za Afrika,eneo la Sahel na upembe wa Afrika ni maeneo ambayo hukumbwa na tatizo la uhaba wa chakula mara kwa mara.
Muungano wa Afrika umekosolewa kwa kujikokota katika kuchukua hatua kukabiliana na migogoro ya kisiasa Afrika ya Kati na Sudan Kusini.
Muungano huo umemteua Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kama mwenyekiti wake mpya.
Generali Abdel Aziz aliingia mamlakani nchini Mauritania mwaka 2009, baada ya kuongoza matukio mawili ya mapinduzi katika kipindi cha miaka minne. CHANZO BBC SWAHILI

No comments:
Post a Comment