Sudan mbili zajadili ulinzi wa mafuta
Sudan na Sudan Kusini zimejadili swala
la kushirikiana katika kushika doria ili kulinda visima vya mafuta
Sudan Kusini ambako waasi wanatishia usalama.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini.
Marais
wa nchi hizo mbili wameanza mazungumzo ya kupeleka kikosi cha ulinzi ili
kulinda visima vya mafuta Kusini ambako waasi wamezusha vurugu kwa
karibu wiki nne sasa.
Taarifa hii inakuja baada ya Rais wa
Sudan Omar Bashir kwenda mjini Juba kwa mashauriano na Rais Salva Kiir
kuhusu mzozo wa kisiasa unaotokota nchini humo.
Mgogoro huo kati ya wafuasi wa Rais
Kiir na hasimu wake Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa bwana Kiir
ingawa alifutwa kazi pamoja na mawaziri wengine wa serikali.
Takriban watu 1,000 wameuawa kwenye mgogoro huo uliozuka tarehe 15 mwezi Disemba.(P.T)
No comments:
Post a Comment