MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE AVAMIWA, APIGWA, ATUPWA UNUNIO

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya
Temeke na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Joseph Yona (33),
amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio
Kawe jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mashuhuda wa tukio hilo wanadai walisikia kelele za mtu kupigwa saa tisa usiku.
Mwenyekiti huyo anadai alichukuliwa nyumbani kwake Mtoni Kwa Aziz
Ally na watu wasiojulikana waliokuwa na gari kama la polisi wakidai
wananipelekea kituoni kabla ya kuanza kunishambulia kisha kunitupa.
No comments:
Post a Comment