TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, January 23, 2014

MKUTANO KUHUSU MZOZO WA SYRIA WAANZA USWIZI.

BAN_KI_MOON_4cc14.jpg
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameziambia pande mbili zinazozozana nchini Syria kuwa wakati umefika kwao kufanya mashauriano ya kusitisha mzozo unaokumba taifa hilo.
Akizungumza siku moja baada ya siku ya kwanza ya mkutano wa amani unaofanyika nchini Uswisi, Bwana Ban amesema kuwa lazima raia wa Syria waungane ili kuokoa taifa lao na kuwalinda watoto. (R.M).

Awali, wajumbe wa Seriklai na wale wa Baraza la Upinzani walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza, tangu mzozo huo uanze miaka mitatu iliyopita.
Wajumbe hao walishutumiana, kuashiria mgawanyiko mkali kuhusu ikiwa rais Bashar al Assad, anapaswa kuwa na juku katika serikali ya mpito.
Mabalozi wa mataifa ya magharibi wamesema kuwa uhasama huo unaweza kuhujumu, mazungumzo rasmi yatakayoanza siku ya Ijumaa.
Mjumbe wa wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Lakhdar Brahimi, amesema atashauriana na pande hizo mbili baadaye hii leo ili kujadili jinsi mazungumzo hayo yatakavyoendelea.
Balozi wa Syria, katika Umoja wa Mataifa Bashar Ja'afari amelalamika kuwa kumekuwa na mapungufu katika mazungumzo hayo kwa sababu ya kutokuwepo kwa Iran, nchi inayowaunga mkono kwa sababu wajumbe wengine wanaohdhuria mkutano huo ni wapinzani wa serikali.
Chanzo, bbc swahili.com

No comments:

Post a Comment