Champagne ahaidi mabadiliko makubwa FIFA
Mgombea wa kiti cha urais wa shirikisho la mchezo wa soka duniani
FIFA, Jerome Champagne, amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa kutoa kadi
ya chungwa wakati wa mechi za soka, ili kuruhusu marefa wa mechi
kuwaruhusu wachezaji waliofanya madhambi kuondolewa uwanja kwa muda.
(HM)
Champagne mwenye umri wa miaka hamsini na tano kutoka Ufaransa,
aliyasema hayo siku ya Jumatatu wakati alipoanzisha kampeini yake ya
kumrithi Sepp Blatter kama rais wa FIFA.
Amesema ikiwa atashinda atapendekeza vilabu vya soka kuadhibiwa ikiwa wachezaji wake watahoji maamuzi ya refa na vile vile kuchunguza uwezekan wa kutumia technolojia kutatua maamuzi muhimu.
Uchaguzi wa urais wa FIFA utafanyika mjini Zurich Juni mwaka wa 2015.
Miongoni mwa mapendekezo mengine aliyoyasema ni kuthibiti idadi ya wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa na vilabu, kutangazwa kwa mshahara wa rais wa FIFA na maafisa wengine wakuu.
Aidha amehaidi kuwa atafutilia mbali sheria ya sasa inayotoa adhabu tatu kwa mchezaji ambaye atafadha madhambi katika eneo la hatari.
Kuambatana na sheria ya sasa mchezaji yeyote anayefanya kosa katika eneo la hatari, hupewa kadi nyekundi moja kwa mojha na pia kupigwa marufuku ya kutocheza mechi mbili zijazo. Chanzo: bbcswahili

No comments:
Post a Comment