BANDARI DAR KUPAKUA MIZIGO TANI MILIONI 18
BANDARI
ya Dar es Salaam kwa kupitia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN),
inatarajia kupakua mizigo tani milioni 18 ifikapo mwaka 2015 kutoka tani
milioni 13.5 wanayopakua sasa.
Aidha,wanatarajia
kuboresha bandari ndogo za kwenye maziwa kuongeza ufanisi wa kutoa
mizigo ikiwemo kuongeza ufanisi wa Usafiri wa Reli ambao kwa sasa unatoa
bandarini asilimia 1.2 ya mizigo tu.
Meneja wa
Bandari ya Dar es Salaam, Awadhi Massawe alimweleza hayo Waziri Mkuu wa
Finland, Jyrki Katainen alipotembelea bandari hiyo, ikiwa sehemu ya
ziara yake ya siku mbili nchini iliyomalizika jana.
Massawe
alikuwa akielezea mafanikio na changamoto zinazoikabili bandari hiyo na
kubainisha kuwa ifikapo mwaka 2028 wanatarajia kupakua tani milioni 41.5
za mizigo.
Akizungumza
bandarini hapo, Katainen alisema amefurahishwa na uamuzi wa Serikali
kuipa kipaumbele uboreshaji wa bandari kupitia mpango wa BRN kwani ikiwa
na uwezo wa kutoa stahili pia biashara nchini itakuwa imara.
Wakati
huo huo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyere aliwahakikishia
watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam kuwa ni salama katika
usafirishaji, uhifadhi na udhibiti wa kemikali mbalimbali hasa zile za
salfa.
Alisema
tangu mwaka 2003 kumekuwa na sheria ya kudhibiti usafirishaji na
uhifadhi wa kemikali nchi nzima. Katika bandari hiyo alisema upo
uangalizi maalumu.
CHANZO:HABARILEO
No comments:
Post a Comment