Mazungumzo kuhusu Sudan Kusini yaanza
Mazungumzo ya kupatanisha pande mbili
zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini na kusitisha vita, yameanza
mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika
wizara ya mambo ya nje nchini Ethiopia, wajumbe kutoka kanda ya Afrika
Mashariki wananuia kusuluhisha mgogoro huo wa kisiasa ambao umekuwa
ukitokota kwa takriban wiki tatu.
Hata hivyo mazungumzo ya ana kwa ana yangali kuanza kati ya pende zinazozozana yangali kuanza.
Waakilishi kutoka pande zinazozozana
wanakutana na wajumbe wa kikanda wanaoendesha mazungumzo hayo ingawa
haijulikani ikiwa vingozi wa Sudan Kusini wenyewe watakutana ana kwa
ana.(P.T)
Mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo
wameachwa bila makao kufuatia mapigano hayo kati ya majeshi ya Rais
Salva Kiir na yale ya hasimu wake ambaye alikuwa makamu wake wa Rais
Riek Machar
Wakati huo huo, ubalozi wa Marekani, katika mji mkuu wa Sudan Kusini,Juba unaendelea na shughuli ya kuwahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo kutokana na mzozo unaoendelea.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa hautarajii raia wa Marekani wanaofanya kazi na shirika lake lolote kuondoka.
Waasi wakiongozwa na makamu wa rais wa zamani Riek Machar wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali tangu mwezi uliopita.

No comments:
Post a Comment