MESSI BORA, HATA ASIPOPATA TUZO
MLINZI wa kulia wa Barcelona, Dan
Alves amedai kuwa anaamini Lionel Messi ataendelea kuwa mchezaji bora
zaidi kwa sasa ulimwenguni hata kama hatapata tuzo ya mwanasoka bora wa
dunia. (HM)
Mastaa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Franck Ribery wa Bayern Munich wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo, lakini Alves anaamini kuwa haitabadilisha lolote na Messi ataendelea kuwa mchezaji bora zaidi wa zama hizi.
"Tuzo ya mwanasoka bora wa dunia inachosha kidogo kwa sababu imehamishwa mahala pake. Imepelekwa katika eneo la mawazo ya watu, nje ya uwanja wa soka. Lakini kama tukitazama mambo ya uwanjani nadhani Lionel anawasukuma wengine katika nafasi ya pili," alisema Alves.
Kwa misimu minne mfululizo, Messi amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa dunia na ingawa msimu huu hapewi nafasi kubwa kutokana na kuwa majeruhi kwa kipindi kirefu, lakini bado amechaguliwa katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo. Chanzo: mwanaspoti
No comments:
Post a Comment