Walichokisema wazazi wa wasichana waliotekwa Nigeria
Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara nchini Nigeria wamekanusha madai kuwa wanaingiza siasa kwenye kilio chao kuitaka serikali ya nchi hiyo iwaokoe watoto wao.
Hii ni baada ya wazazi hao kukataa wito wa kukutana na rais Goodluck Jonathan hapo jana baada ya kushinikizwa na mwanaharakati mdogo kutoka Pakistan Malal Yousafzai.
Rias Jonathan amesema ni aibu kubwa kwa wazazi hao kuruhusu kushinikizwa na mitandao ya kijamii hasa kutokana na kampeni yao kwenye mitandao yenye kauli mbiu, “Bring Back Our Girls”.
Lakini msemaji wa wazazi hao, amesema kuwa walikataa kukutana na Rais kwa sababu jamii ya watu wa Chibok haikuwa imewapa ruhusa kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment