Muda wa majadiliano na Iran waongezwa
Viongozi wajadiliana na kuhusu mpango wa nuklia wa Iran
Wawakilisha wa mataifa sita yenye
uwezo mkubwa duniani pamoja na Iran wameongeza kwa miezi mengine minne
makubaliano ya mpango wa nuklia wa Iran.Wajumbe wanaokutana mjini Vienna wamesema kuwa tofauti zilizopo ni kubwa mno kuafikiwa kabla ya kukamilika kwa siku ya mwisho hapo kesho.
Katika taarifa iliosomwa kwa pamoja, afisa, anayesimamia sera za kigeni katika muungano wa Ulaya Catherine Ashton pamoja na waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Javad Zarif wamesema kuwa licha ya hatua muhimu kupigwa kuna tofauti kubwa.
Majadiliano sasa yataendelea hadi Novemba 24. Wakati huo Marekani itatoa takriban dola billioni 3 za Mali ya Iran ili taifa hilo libadilishe utajiri wake wa Uranium kuwa mafuta.
Katika makubaliano ya mda yalioafikiwa mwezi Novemba mwaka uliopita ,Iran ilikubali kusitisha uzalishaji wake wa Uranium kwa lengo la kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa vilivyoigharimu takriban dola bilioni saba.(P.T)
No comments:
Post a Comment