BRAZIL WAIPIGA COLOMBIA 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI
Beki wa
Brazil, David Luiz aliachia shuti kali la mpira wa adhabu na kufunga
bao la pili na la ushindi.ULIKUWA usiku mkubwa kwa Wabrazil wakishuhudia
vijana wao wa Samba wakicheza mechi ngumu ya robo fainali ya kombe la
dunia dhidi ya timu ya Colombia.Haikuwa rahisi kuwazuia Wabrazil
waliokuwa na morali ya kushinda mechi ya leo na kuungana na Ujerumani
iliyofuzu nusu fainali kwa kuifunga Ufaransa bao 1-0 katika mchezo wa
kwanza.Usiku huu kumekuwepo na maendeleo, shukurani kwa bao la mapema la
Thiago Silva (dakika ya 7) lililowachanganya Colombia.Ulikuwa mchezo
mkali na wenye kasi kwa dakika zote 90, lakini bao la pili lililofungwa
na David Luiz kwa shuti kali la mpira wa adhabu katika dakika ya 68
liliwaamusha Wabrazil kwa mara nyingine tena.Alikuwa kijana mkali, James
Rodriguez aliyeifungia Colombia bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa
penati katika dakika ya 80, lakini yote kwa yote, Wacolombia ndio `bai
bai` tena.
Luiz akishangilia baada ya kufunga goli kwa shuti la mpira wa adhabu lililomuacha kipa wa Colombia, David Ospina akiambulia manyoya tu.
David Luiz akimshukuru Mungu wake baada ya kufunga, huku Paulinho akimtazama kwa tabasamu. (P.T)
Bao la ufunguzi: Thiago Silva akifunga bao la kuongoza la mapema dhidi ya Colombia.
Beki wa Brazil, Thiago Silva akishangilia baada ya kufunga.
Kikosi cha Brazil: Julio Cesar, Maicon, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Fernandinho, Paulinho, Oscar, Neymar, Hulk, Fred.
Wachezaji wa akiba: Jefferson, Dani Alves, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Victor.
Wafungaji: Thiago Silva, 7, David Luiz, 68.
Kikosi cha Colombia: Ospina, Zuniga, Zapata, Yepes, Armero, Guarin, Sanchez Moreno, Cuadrado, Rodriguez, Ibarbo, Gutierrez.
Wachezaji wa akiba: Vargas, Arias, Carbonero, Aguilar, Mejia, Balanta, Bacca, Ramos, Quintero, Martinez, Valdes, Mondragon.
Mfungaji: Rodriguez (pen), 80.
Mwamuzi: Carlos Velasco Carballo (Spain)
No comments:
Post a Comment