TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 16, 2014

Uwezekano wa janga la Ukimwi kutokomezwa 2030

aids2
Habari njema ni kwamba kuna uwezekano wa Janga la Ukimwi kudhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la kupambana na Ukimwi.
Shirika hilo linasema idadi ya maambukizi mapya na wanaokufa kutokana na Ukimwi imeendelea kushuka.
Hata hivyo jitihada zaidi za kimataifa zinahitajika kwani zilizopo hazitoshi kumaliza janga hilo.
shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa watu milioni 35 duniani wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa maambukizi mapya milioni 2.1 yalitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.
Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

No comments:

Post a Comment