BANGI RUKSA SASA WASHINGTON
Uuzaji wa
bangi kama ulevi wa starehe utaanza kuuzwa rasmi hii leo katika jimbo
la Marekani la Washington. Hili ni jimbo la pili nchini humo kuhalalisha
bangi kwa matumizi ya burudani, baada ya jimbo la Colorado kufanya
hivyo. Mapato ya kodi kutokana na uuzaji wa bangi katika jimbo la
Colorado yamefikia dola milioni kadhaa sasa. Mchakato huo utadhibitiwa
kwa makini katika jimbo la Washington. Maduka ishirini na tano tu ndio
yamepata leseni ya kuuza mpaka sasa, ingawa maafisa wanasema idadi hiyo
huenda ikaongezeka na kufikia maduka takriban mia moja. Majimbo mengine
23 nchini Marekani tayari yanaruhusu uuzaji na ununuaji wa bangi lakini
kwa sababu za kitabibu. (BBC)(FRIDAY SIMBAYA)
No comments:
Post a Comment