TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 9, 2014

Ni Argentina dhidi ya Ujerumani Fainali 


Kipa wa Argentina Sergio Romero alikuwa Nyota wa mechi hiyo
Argentina imejukatia tikiti ya kufuzu kwa fainali yake ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo itachuana Ujerumani.
Argentina ilikuwa imetoka sare tasa baada ya muda wa kawaida na ule wa Ziada na hivyo kulazimu mechi hiyo kuamulia kwa mikwaju ya penalti.
Kipa wa Argentina Sergio Romero ndiye aliyekuwa nyota katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwaju miwili na kuipa Argentina Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Uholanzi.

Kipa wa Argentina Sergio Romero alikuwa Nyota wa mechi hiyo
Romero aliokoa mikwaju ya Ron Vlaar na Wesley Sneijder.
Wafungaji wa Argentina walikuwa ni Lionel Messi,Ezequiel Garay Sergio Aguero na kisha Maxi Rodriguez.
Argentina sasa Itachuana na Ujerumani ambayo iliweka historia kwa kuinyuka Brazil mabao 7-1katika nusu fanali.(P.T)

Kocha wa Argentina Alejandro Sabella amefurahia kufuzu kwa fainali.
Uholanzi ambayo sasa imeshindwa kutwaa kombe la dunia hata baada ya kufuzu kwa nusu fainali tatu mfululizo itachuana dhidi ya wenyeji Brazil siku ya jumamosi kuamua mshindi wa tatu.
Brazil ilipata kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani siku ya Jumanne.
Penalti ndizo zitakazoamua nani kati ya Uholanzi na Argentina atakutana na Ujerumani katika fainali.
00:45 Mpira umekwisha .Sasa ni dakika 30 za muda wa ziada.

Argentina 0-0 Uholanzi 85''
00:43 Hakuna mechi ya Nusu fainali ya kombe la dunia ambayo imeishia sare tasa hata baada ya muda wa ziada.
00:42 Argentina 0-0 Uholanzi 82''
00:40 Argentina wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili kwa mpigo.
00:06 Demichelis anaoneshwa kadi ya Njano baada ya kumwangusha Arjen Robben
00:05Uholanzi 0-0 Argentina 45'' Kipindi cha pili kimeanza .

Mshambulizi wa Argentina Messi amezimwa
23:45+2Kipindi cha kwanza kimekamilika .
23:45 +1 Kufikia wakati kama huu hapo jana Ujerumani ilikuwa imemfunga Brazil mabao 5-0

Mashabiki katika uwanja wa sao Paolo
23:45 Uholanzi 0-0 Argentina 45''
23:44 Martins Ndi (uholanzi) aoneshwa kadi ya kwanza ya manjano
23:23 Kona nyengine kuelkea upande wa Uholanzi ,duh unatoka nje na inakuwa ni Goalkick
23:20 Kona ya kwanza kuelekea upande wa Uholanzi,,,lakini Wapi inazimwa
23:20 Argentina 0 -0 Uholanzi
23:14 Messi ndiye anaupiga lakini kipa Cillessen wa Uholanzi anaudaka bila wasiwasi

Sao Paolo Argentina vs Uholanzi
23:13 Perez anaopatia Argentina Freekick ya pili nje tu ya eneo
23:10 Argentina 0-0 Uholanzi
23:09 Messi anapata FREEKICK ya kwanza kuelkea kwa Argentina
23:00 Mpira unaanza hapa sao Polo Argentina dhidi ya Uholanzi .
22:59 Perez amechukua nafasi iliyowachwa na Di Maria upande wa Argentina
22:59 Van Persiena De Jong wanaanza kwa upande wa Uholanzi
22:57 Wimbo wa taifa unachezwa hapa Sao Paolo

Shabiki wa Uholanzi
22:55
22:54Wachezaji wa Argentina Sergio Aguero na Marcos Rojo wamerejea
22:54 Mshambulizi wa Bracelona Lionell Messi atakabidhiwa majukumu mahsusi ya kuifikisha Argentina katika fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 1990.
22:53 Argentina wanatatizika kwa kumkosa mchezaji wa kutegemewa Angel Di Maria ambaye amejeruhi paja
22:52 Uholanzi tofauti na Argentina imefuzu kwa fainali ya kombe la dunia mara mbili zilizopita ikimaliza ya pili mara mbili mfululizo .

Mashabiki wa Argentina wakisubiri mechi hiyo ya kihistoria
22:51 Argentina inatafuta tiketi yake ya kwanza ya Fainali tangu mwaka wa 1990
22:50 Argentina inachuana na Uholanzi katika mechi ya pili ya nusu fainali ya kombe la dunia Brazil
Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment