UJERUMANI NA CHINA :UHUSIANO MAHSUSI?
Kansela Angela Merkel na Rais wa China Xi Jinping
China na
Ujerumani zinatarajia kutiliana saini mikataba kadhaa wakati wa ziara ya
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel inayoanza Jumapili nchini China.
Ni katika mwezi wa Machi tu ambapo Rais wa China Xi Jinping aliafanya ziara nchini Ujerumani.
Na mapema
mwaka huu Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier
alikuwapo China kwa ajili ya ziara.Na katika msimu wa mapukutiko baraza
lote la mawaziri la China litakuwapo nchini Ujerumani kwa ajili ya
mashauriano ya kiserikali. Licha ya hatua hizo zote zaira ya Kansela wa
Ujerumani inafuatia.
Hakuna
kiongozi mwengine yeyote wa Ulaya anaekutana na viongozi wa China mara
kwa mara kuliko Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Uhusiano baina ya
Ujerumani na China unasonga mbele kwa nguvu.Na ili kuidumisha kasi
Kansela Merkel sasa anaitembelea China.(P.T)
Katika
ziara hiyo mikataba kadhaa itatiwa saini baina ya Ujerumani na China juu
ya mambo ya tekinolojia, elimu na utamaduni. Kansela Merkel ataianzia
ziara yake ya siku tatu katika jimbo la Sichuan la kusini magharibi mwa
China.Jimbo hilo lina idadi ya wakaazi sawa na Ujerumani.
Kwa muda
wa karibu miaka 10 Ujerumani imekuwa inakimu ubalozi katika mji mkuu wa
jimbo hilo, Chengdu. Sababu ni kwamba mji huo ni daraja la kuingilia
katika jimbo la Sichuan kwa makampuni ya Ujerumani.Jimbo hilo la
magharibi linahesabika kuwa na maendeleo hafifu. Makampuni karibu 160 ya
Ujerumani yanawakilishwa katika jimbo hilo.Kansela Merkel ataitembelea
kampuni ya magari ya VW.
Jumapili
jioni Kansela Merkel ataenda Beijing ambako atakutana na Waziri Mkuu wa
China Li Keqiang. Hapo Jumatatu kiongozi huyo wa Ujerumani atakutana na
Rais Xi -Jinping ambae pia ni Mwenyekiti wa chama cha kikomunisti
kinachotawala China.
Profesa
wa masuala ya Ujerumani kwenye chuo kikuu cha lugha za kigeni cha mjini
Beijing Liu Liqun anataraji kwamba viongozi hao watayazungumzia masuala
ya kiuchumi.
Kitovu cha mazugumzo ni masuala ya kiuchumi
Kwa mara
ya kwanza kamati mpya ya mashauriano ya masuala ya kiuchumi itakutana
mjini Beijing ambapo Kansela Merkel na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang
watakuwapo.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa taasisi ya mitaala ya China
Sebastian Heilmann, kamati hiyo itayafafanua masuala ya kiuchumi
yanayozihusu nchi mbili hizo na kutoa mapendekezo kwa viongozi. Serikali
za Ujerumani na China zitayashughulikia mapendekezo hayo kwa kuchukua
hatua thabiti.
Hati miliki
Katika
mahojiano na DW, mtaalamu wa China wa masuala ya Ujerumani Liu Liqun
amekiri kwamba yapo matatizo katika upande wa China kuhusiana na ulinzi
wa hati miliki.Amesema kwamba katika miaka ya hivi karibuni mengi
yameboreshwa lakini hatua zilizochukuliwa hazijatosha. Amesema matatizo
yanaweza kutokea katika utekelezaji wa mradi wa uhaulishaji unaopewa
kipaumbele pia na China.
Mwaka ujao unaazimiwa kuwa wa kuutekeza mradi wa ushirikiano katika uhaulishaji baina ya Ujerumani na China.
Haki za binadamu
Ilifahamika
hata kabla ya Merkel kuanza ziara kuwa suala la haki za binadamu
litazungumziwa .Katika suala hilo bado pana mapungufu mengi katika
upande wa China. Hata hivyo masuala hayo yatajadiliwa kwenye vikao vya
faragha kwa uthabiti na hata kwa hoja za mabishano ,mkasa kwa mkasa
utajadiliwa.
Kwa
mujibu wa taarifa Kansela Merkel atampigania mwanaharakati Ai Weiwei ili
apewe kibali cha kuondoka nchini China. Kwa muda wa miezi kadhaa sasa
mwanaharakati huyo ambae pia ni msanii amekuwa anatumai kuondoka China
na kuenda Ujerumani.Msanii huyo bado ameshikiliwa mjini Beijing na idara
husika. Kwa sasa maonyesho ya kazi zake za kisanii ambayo ni makubwa
kabisa kuwahi kufanyika yanaendelea mjini Berlin.
Mwandishi von Hein,Matthias
Tafsiri:Mtullya Abdu
Mhariri:Ssessanga Iddi
Tafsiri:Mtullya Abdu
Mhariri:Ssessanga Iddi
Chanzo:http://www.dw.de/
No comments:
Post a Comment