BEI ZA MAFUTA NA UMEME ZAPANDA MISRI
Bei za
mafuta na umeme zilizopanda zimeanza kutekelezwa nchini Misri huku
serikali ikianza kukata ruzuku yake mbali na kupunguza matumizi ya
bajeti yake ili kufufua uchumi ulioathiriwa na mgogoro wa kisiasa wa
miaka kadhaa.
Baadhi ya bei za mafuta zinadaiwa kupanda kwa asilimia 78 huku bei ya umeme ikipanda maradufu katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa sasa serikali inauza umeme kwa nusu ya gharama ya uzalishaji wake.
Kukatika
kwa umeme nchini Misri limekuwa jambo la kawaida na maafisa wanasema
kuwa gharama ya juu ya ruzuku imelemaza ukarabati na upanuzi wa mitambo
ya kuzalisha umeme.
Waandishi
wanasema kuwa kupanda kwa bei ya umeme nchini humo ni hatua mojawapo ya
serikali katika kile kinachotarajiwa kuwa marekebisho ya kisiasa kwa
ruzuku zinazosimamia Mafuta,Uchukuzi,chakula na kilimo.(P.T)
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment