CAG amuita Kafulila kutoa ushahidi sakata la IPTL
Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh
Mkaguzi
na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) amemuandikia barua mbunge wa
Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila akimtaka kufika ofisi za
taasisi hiyo Julai 23 mwaka huu, akiwa na ushahidi wote kuhusu tuhuma za
ufisadi wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Kafulila
aliibua kashfa hiyo wakati wa Bunge la Bajeti alipodai kuwa Sh200
bilioni zilizokuwa kwenye akaunti ya escrow, ambayo ilifunguliwa kuweka
fedha wakati mgogoro baina ya IPTL na Shirika la Umeme (Tanesco) ukiwa
mahakamani kusubiri kutolewa uamuzi, zilichotwa kifisadi na kutaka Bunge
liunde kamati huru kuchunguza.
Hata
hivyo, Bunge lilimuagiza CAG na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) kuchunguza tuhuma hizo za uchotaji wa fedha hizo.(P.T)
Jana CAG
Ludovick Utouh alisema kuwa wamemwandikia barua mbunge huyo wakimtaka
aende kutoa ushahidi kuhusu sakata hilo, huku akisisitiza kuwa Kafulila
siyo mtu wa kwanza kuhojiwa na ofisi yake kuhusu suala la IPTL.
"Lengo
letu ni kukusanya ushahidi wote na kusikiliza watu wanaojua kuhusu IPTL
ili tuweze kujua ukweli wa hili jambo," alisema Utouh.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Kafulila alisema kuwa amepewa ujumbe kutoka ofisi
hiyo jana mchana na kuelezwa kuwa barua yake ya kuitwa kutoa ushahidi
huo ametumiwa kupitia sanduku lake la Posta.
Kuitwa
kwa Kafulila na CAG kumekuja ikiwa zimepita siku tatu tangu IPTL
ilipomfungulia mashtaka mbunge huyo dhidi ya tuhuma alizozitoa za wizi
wa pesa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyoko Benki Kuu (BoT).
Kafulila
amefunguliwa kesi ya madai Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na IPTL
kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited
(mlalamikaji wa pili) na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder
Sigh Seth (mlalamikaji wa tatu), Julai 13 mwaka huu.
Katika
kesi hiyo namba 131 ya mwaka 2014, walalamikaji kwa pamoja wanaiomba
mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe fidia ya jumla ya Sh310 bilioni
kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia pesa kwa
njia zisizo halali.
"Ofisi ya
CAG wameniita na nimewakubalia. Kikubwa nitawaeleza kwanza namna
ambavyo mchakato mzima wa PAP kumiliki IPTL ulivyoambatana na uvunjifu
wa sheria ya fedha (Finance Act 2012.sec29)," alisema.
Kafulila
alisema jambo jingine atakalowaeleza ni jinsi ambavyo makubaliano ya
kutoa fedha hizo yalivyokuwa na nia ovu kwani sehemu ya makubaliano hayo
yanasomeka kwamba mchakato huo uwe siri baina ya pande mbili kwa maana
ya IPTL na PAP (ambayo iliinunua IPTL).
"Pia kwa
upande mmoja na Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) na IPTL kwa upande
wa pili. Hoja ya kujiuliza ni kwanini kipengele cha siri kama utoaji
fedha hizo haukuwa uamuzi ovu?" alihoji.
Kwa
mujibu wa sheria za akaunti ya escrow, fedha zinazowekwa hutakiwa kutoka
kwa idhini ya pande zote mbili kwa ajili ya malipo ambayo ni lazima
yafanywe wakati kesi ikiendelea na iwapo kesi itamalizika, fedha hizo
zitalipwa kwa mujibu wa hukumu.
Zaidi ya
Sh400 bilioni zilikuwa zimewekwa kwenye akaunti hiyo wakati kukiwa kuna
mgogoro wa kisheria baini ya wabia wa zamani wa IPTL (VIP Engeneering
and Marketing na Mechmar Corporation ya Malaysia) kwa upande mmoja,
Tanesco na IPTL kwa upande mwingine, lakini baada ya kikao cha pamoja
baina ya wabia hao, Tanesco na Wizara ya Madini, zaidi ya Sh200 bilioni
zilitolewa na PAC ikalipwa
No comments:
Post a Comment