SERIKALI YAKILI MATATIZO YA WAALIMU KIKWAZO CHA ELIMU
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa
SERIKALI
imekiri kuwa matatizo mbalimbali katika sekta ya elimu yanasababisha
baadhi ya walimu kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo hali
inayochangia kushasha elimu.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa ripoti ya hali ya elimu Tanzania iliyoandaliwa na
Shirika lisilo la Kiserikali la Twaweza, Meneja Mawasiliano, Mipango na
Usimamizi wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa,
alisema matatizo mbalimbali yanayowakabili walimu pamoja na serikali
kuchelewa kuwalipa mishahara kwa wakati ni kikwazo kwa elimu.(Martha Magessa)
Katika
uzinduzi huo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa,
jijini Dar es Salaam Rugaba alisema kitendo hicho kimesababisha baadhi
ya walimu kutokuwa na moyo wa kufundisha, hali iliyosababisha baadhi yao
kushindwa kutimiza majukumu.
"Sekta ya elimu ina changamoto nyingi ambazo zinatokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya walimu kutokuwa na moyo wa kufundisha.
"Hali
hiyo inasababisha idadi kubwa ya wanafunzi kufeli na wengine kukosa
masomo kutokana na walimu kutoingia madarasani,"alisema Rugaba.
Aliongeza
kuwa mbali na matatizo hayo, pia kuna changamoto ya migogoro ya walimu
inayotokana na ukosefu wa nyumba, madeni wanayoidai serikali na
mishahara duni.
Alifafanua
kuwa kutokana na hali hiyo, serikali ilianzisha mpango wa Matokeo
Makubwa sasa(BRN) ili kuangalia matatizo hayo na kutafuta mbinu ya
kuyatatua.
Hata
hivyo Rugaba alisema baada ya kuona hivyo, serikali imejitahidi kulipa
madeni ya walimu kwa zaidi ya asilimia 65 hali iliyosaidia kulipunguza
deni hilo kwa kiasi kikubwa.
Katika
kutatua matatizo ya walimu ili kuboresha elimu nchini, alisema serikali
imepanga kujenga nyumba za walimu katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwa
ni pamoja na kuwapa motisha wale watakaofanya vizuri kwenye shule zao
ili kuwahamasisha wengine waweze kujituma zaidi.
Alisema
walimu ambao shule zao hazitafanya vizuri kwenye mitihani, watawaita na
kuzingumza nao ili waweze kujua tatizo lililopo na kulifanyia kazi.
Kwa
upande wake mtafiti kutoka Twaweza, Constantine Manda alisema kuwa baada
ya kufanya utafiti katika shule mbalimbali nchini walibaini kuwa
asilimia 34 ya walimu ndio wanaoingia madarasani huku asilimia 38
hawaingii kabisa.
Alisema hali hiyo inamaanisha kuwa ni walimu watatu kati ya 10 ndio wanaoingia darasani katika muda wa vipindi.
Alisema
tatizo hilo linasababishwa na waalimu kukosa moyo wa kufundisha,
migogoro baina yao na serikali pamoja na hali ngumu za maisha.
Alisema
kutokana na hali hiyo, serikali inapaswa kushughulikia matatizo hayo
ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo yaliyopo hali itakayosaidia
kupunguza ukubwa wa tatizo.
CHANZO:MTANZANIA
No comments:
Post a Comment