NEYMAR KUKOSA KOMBE LA DUNIA
Mchezaji Neymar baada ya kupata jeraha
Nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha.
Mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.
Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Brazil
pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago
Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya
mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya
habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara
za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .(A.I).
No comments:
Post a Comment