NIGERIA IMEWAKAMATA BOKO HARAM WANAWAKE
Jeshi
nchini Nigeria linasema limewakamata wanawake watatu ambao walikua
wanawaandikisha wafuasi wanawake kwa kundi la siasa kali za Kiislamu la
Boko Haram.
Inadaiwa wanawake hao waliwalenga wajane na wasichana wadogo wakiwaahidi kuwachumbia kwa wafuasi wa Boko Haram.
Mwaandishi
wa BBC Will Ross akiwa Abuja anasema inaelekea Boko Haram inajaribu
kuwashawishi wanawake washiriki vilivyo katika mapambano yao.
Mwezi
uliopita mshambuliaji mwanamke wa kujitoa mhanga alifariki alipojaribu
kuishambulia kambo ya kijeshi katika jimbo la Gombe - tukio la kwanza
aina hiyo nchini Nigeria.
Bomu hilo lililipuka alipokua akipekuliwa katika kituo cha usalama . Mwanajeshi mmoja pia aliuwawa.
Wanawake
pia ni miongoni mwa wale waliokamatwa na kuzuiliwa katika miji ya
Maiduguri kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo Boko Haram wanaungwa mkono
kiasi .
Jeshi la Nigeria limesema wanawake watatu iliowakamata walikuwa ni wa tawi la upelelezi.
Ilisemekana mmoja wao alikua ni mjane wa mpiganaji wa Boko Haram.
Kundi
hilo la wanaharakati wa Kiislamu bado linawashikilia zaidi ya wasichana
wa shule 200 iliowakamata mnamo mwezi wa Aprili katika mji wa Chibok
katika jimbo la Borno .
Boko Haram inadai wapiganaji wake na jamaa zao waachiliwe kwa kubadilishana na wasichana.Serikali imelikataa dai hilo.(P.T)
No comments:
Post a Comment