CAR:Waasi wataka nchi kugawanywa
kundi la wapiganaji nchini CAR
Waasi
katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wamekataa makubaliano ya kusitsisha
vita na kutaka taifa hilo ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.
Afisa
mkuu wa waasi wa kundi la kiislamu la Seleka ameiambia BBC kwamba
wapiganaji wake watapuuza makubaliano hayo yalioafikiwa siku ya jumatano
kwa kuwa yalifanywa bila wao kuhusishwa.(P.T)
Joseph
Zoundeiko amewalaumu Wakristo wa Kusini mwa taifa hilo kwa kushindwa
kuleta amani na kusema kuwa taifa hilo ni sharti ligawanywe mara mbili.
Mapigano
ya miezi kadhaa kati ya makundi ya Wakristo na yale ya Waislamu katika
taifa hilo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku mamilioni
wakiwachwa bila makao.
Kundi la waasi wa Seleka lilivunjwa rasmi mwaka uliopita.
lakini
kundi la Human Rights Watch linasema kuwa wapiganaji hao wameelekea
katika maeneo ya mashambani na kwamba wameanza kuzishambulia jamii za
Wakristo.
Wakristo na wamelipiza kisasi na hivyobasi kusababisha maafa zaidi kutoa pande zote mbili.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment