TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, July 9, 2014

UN - Gaza inatishiwa kuangamizwa 

Ban Ki Moon wa umoja wa mataifa
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-moon, ameonya kuwa hali huko Gaza imo ukingoni na huenda ikawa mbaya kiasi cha kutoweza kudhibitiwa.
Bwana Ban amesema eneo hilo haliwezi kuhimili vita vingine na ametoa wito kwa pande zote zisitishe ghasia.(P.T)
Amelitaka kundi la Hamas lisite kufyetua makombora dhidi ya Israel na ameiomba serikali ya Israel kujizuia na iheshimu jukumu lake la kimataifa la kuwalinda raia.
Katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amepangiwa kufanya mkutano wa dharura Alhamisi na baraza la Usalama la Umoja huo kujadili mzozo wa Gaza.
Benjamin Netanyahu , waziri mkuu wa Israel
Awali, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa onyo kuwa nchi yake iko tayari kuimarisha oparesheni zake dhidi ya kile alicho kitaja kuwa uvamizi wa kigaidi ndani ya Gaza.
Alitaka mashambulio ya makombora yasitishwe mara moja hidi ya ardhi yake.
Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment