TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, July 26, 2014

BAHATI BUKUKU APATA AJALI 



Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku amepata ajali ya gari akiwa na dereva wake, Eddy maeneo ya Kongwa Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Akiongea kwa simu Bahati amesema: “Ni Mungu tu aliyetuokoa, tulikuwa tunaelekea Kahama kwenye huduma ghafla tukagongana uso kwa uso na lori, gari yetu aina ya Toyota Nadia  iliruka na kubiringika kama mara tatu hivi, tumetoka tukiwa tumeumia sana.(P.T)
“Hapa siwezi kusimama wala kukaa na dereva wangu kaumia sana mguu. Gari yangu imeumia sana wala huwezi kuamini kama kuna mtu katoka salama.”
Taratibu za kumhamishia Bahati kutoka Hospitali ya Kongwa kuja Muhimbili zinafanywa na ndugu pamoja na marafiki.
Tunakuombea upone haraka Bahati.
Chanzo:http://www.globalpublishers.info/

CAR:Waasi wataka nchi kugawanywa 

kundi la wapiganaji nchini CAR
Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wamekataa makubaliano ya kusitsisha vita na kutaka taifa hilo ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.
Afisa mkuu wa waasi wa kundi la kiislamu la Seleka ameiambia BBC kwamba wapiganaji wake watapuuza makubaliano hayo yalioafikiwa siku ya jumatano kwa kuwa yalifanywa bila wao kuhusishwa.(P.T)
Joseph Zoundeiko amewalaumu Wakristo wa Kusini mwa taifa hilo kwa kushindwa kuleta amani na kusema kuwa taifa hilo ni sharti ligawanywe mara mbili.
Mapigano ya miezi kadhaa kati ya makundi ya Wakristo na yale ya Waislamu katika taifa hilo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku mamilioni wakiwachwa bila makao.
Kundi la waasi wa Seleka lilivunjwa rasmi mwaka uliopita.
lakini kundi la Human Rights Watch linasema kuwa wapiganaji hao wameelekea katika maeneo ya mashambani na kwamba wameanza kuzishambulia jamii za Wakristo.
Wakristo na wamelipiza kisasi na hivyobasi kusababisha maafa zaidi kutoa pande zote mbili.
Chanzo:BBC

Gaza:Israel na Hamas wasitisha vita  

Kiongozi wa Hamas na mwenzake wa Israel
Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wamekubaliana kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu kuanzia leo asubuhi.
Taarifa ya Israel imesema kuwa raia wa Palestina katika eneo la Gaza ambao walikuwa wameonywa kuondoka katika makaazi yao wasithubutu kurudi na kwamba Israel italipiza kisasi iwapo itashambuliwa.(P.T)
Awali serikali ya Israel ilikataa makubaaliano ya kusitisha kwa mda mrefu yaliopendekezwa na waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry .
Bwana Kerry amesema atendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.
Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.
Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30

DIDIER DROGBA ASAINI CHELSEA NA KUUNGANA NA MOURINHO TENA 

article-2705875-1FFB085F00000578-986_634x478
Didier Drogba amekamilisha ndoto za kurejea Chelsea.
Nyota huyo wa Ivory Coast amesaini mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge.
Gwiji huyu alisainiwa kwa mara ya kwanza klabuni hapo na Jose Mourinho kwa dau la paundi milioni 24 mwaka 2004.
Drogba amefichua siri kuwa hakutaka kupoteza nafasi ya kufanya kazi tena na kocha Mourinho kwa mara nyingine tena.
article-2705875-1FFB023200000578-717_634x612
Mshambuliaji huyu wa Ivory Coast amekamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Chelsea. 
Alisema: “Yalikuwa maamuzi rahisi-nisingeweza kupoteza nafasi ya kufanya kazi tena na Jose. Kila mtu anajua mahusiano mazuri niliyokuwa nayo na klabu hii, na mara zote nimekuwa nikijisikia kama nyumbani”. 
article-2705875-1FFAFECB00000578-590_634x354
“Hamu yangu bado ni ileile na naangalia mbele kuisaidia timu hii. Namefurahia sana ukurasa huu mwingine wa maisha yangu ya soka”.(P.T)
Mourinho amewaondoa hofu mashabiki wa klabu hiyo akisisitiza kuwa Muivorycost huyo bado ni mshambuliaji bora katika ulimwengu wa soka.
“Amekuja kwasababu ni miongoni mwa washambuliaji bora Ulaya. Namjua sana na najua kuja kwake hajivunia historia yake au kile alichofanya klabuni miaka ya nyuma”, Alisema Mourinho.
Mchezo wa mwisho kwa Drogba akiwa Chelsea ulikuwa wa UEFA ambao alifunga penati ya ushindi na kutwaa kombe hilo dhidi ya Bayern mwaka 2012.
Chanzo:Shaffihdauda.com

Friday, July 25, 2014

Mwanamke wa Sudan aliehukumiwa kifo kwa kuolewa na Mkristo amewasili Italia

Sudan 1
Huyu wa kwanza kushoto aliembeba mtoto ni Makamu wa waziri wa mambo ya nje ya Italy Lapo Pistelli
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis Alhamisi ya July 24 2014 nchini Italia amekutana na Meriam mwanamke wa Sudan ambae alihukumiwa kunyongwa nchini Sudan kwa kosa la kuolewa na mume Mkristo mwaka 2011.
Meriam na watoto wake wawili akiwemo huyu wa mwisho aliezaliwa gerezani pamoja na mume wake ambae ni raia wa Marekani mwenye asili ya Sudan, waliwasili Italy wakiwa wameongozana na Afisa wa Italia ambae alisaidia kwenye mazungumzo na serikali ya Sudan ambayo iliwashikilia Meriam na mumewe kwa wiki kadhaa baada ya kuwakamata Airport wakiondoka nchini humo.
Video iliyotolewa na Vatican imemuonyesha Pope akimpa Meriam medali pamoja na rozari ambapo baada ya kukutana na Pope, wawili hawa wakiwa na watoto wao watambatana kuelekea nchini Marekani ambako ndiko makazi yao yalipo New Hampshire alikowahi kuishi mume wa Meriam.
New Hampshire Marekani.
New Hampshire Marekani.
Afisa wa Italia aliehusika kuongea na serikali ya Sudan ili familia hii iachiwe, amesema ilibidi wawe wapole kwenye maongezi na ndicho kilichosaidia mwishoni wakaachiwa huru baada ya kushikiliwa pamoja na kwamba Mahakama kuu ya Sudan ilimuachia huru Meriam.
MS3
Meriam mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifo baada ya kukataa amri ya kurudi kwenye dini ya baba yake ambae ni Muislamu ambapo alifungwa gerezani na kujifungulia mtoto wake wa pili hukohuko akiwa amefungwa minyororo mpaka miguuni wakati wa kujifungua.
sudan 3
Waziri wa mambo ya nje wa Italia Federica Mogherini akiwa na mtoto wa Meriam wakati wakiwasili nchini Italy July 24 2014 baada ya kuachiwa huru Sudan.

Wednesday, July 23, 2014

Mlipuko waua 40, Nigeria 


Watu wapata 40, wameuawa katika milipuko mikubwa miwili iliyotokea katika mji wa Kaduna, kaskazini mwa Nigeria. Katika mlipuko wa kwanza wa kujitoa mhanga watu 25 waliuawa, huku wengine 15 wakiuawa katika eneo lililokuwa na msongamano wa watu katika mji wa Kawo.
Shambulio hilo pia lilimlenga kiongozi wa upinzani na kiongozi wa zamani wa kijeshi Jenerali Muhammadu Buhari.
Shambulio la kwanza lilimlenga kiongozi mashuhuri wa kiislam aliyeambatana na wafuasi wake alipokuwa akitoka katika eneo la katikati ya Kaduna alikomaliza kufanya muhadhara kwa ajili ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Maelfu ya watu walihudhuria tukio hilo la mwaka.
Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo, watu 25 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Shambulizi la pili lilimlenga kiongozi wa juu wa upinzani ambaye pia ni rais wa zamani Jenerali Muhammadu Buhari ambako nako wamekufa watu 19. Wote wawili, kiongozi wa kiislam na kiongozi wa upinzani wamenusurika bila kujeruhiwa.
Mwanahabari wa BBC amesema aliona viungo vya binadamu vikiwa vimetapakaa katika eneo kubwa la mlipuko. Kamishina wa polisi wa jimbo la Kaduna Alhaji Umar Usman Shehu amesema mlipuko ulisababishwa na anayehisiwa kujitoa muhanga.
Hakuna kundi lolote lililojitokeza kuhusika na mlipuko huo. Kundi la Boko Haram ambalo bado linawashikilia wanafunzi wasichana 200 kwa takribani siku 100 sasa, limeshafanya matukio ya kulipua mabomu kwa kujitoa muhanga katika miji mingi kaskazini mwa naijeria ukiwamo mji mkuu Abuja.
CHANZO BBC,(A.I).

 

Ajali nyingine ya Ndege yaua zaidi ya 40 


Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Waziri wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11 kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa ndege wanne.
ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na na kunawaka moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu.
Meneja Mkuu wa TransAsia Hsu Yi-Tsung huku akilia, ameomba msamaha kwa ajali hiyo na akaahidi kuongeza juhudi za uokoaji na pia kuwasafirisha ndugu wa waliopoteza maisha kwenda kwenye eneo la tukio.
Siku za hivi karibuni Taiwan imepigwa na upepo mkali uliombatana na Mvua zilizoletwa na kimbunga Matmo, hata hivyo wanaosimamia anga katika eneo hilo wamesema hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza kuzuia ndege kutua.
Habari za kuanguka kwa ndege hii kunakuja wakati visanduku viwili vya kutunzia kumbukumbu ya ndege ya malaysia iliyoangua nchini Ukraine tarehe 17 mwezi huu vikiwa vimefika mikononi mwa wataalamu wa masuala ya anga ili kuchunguza ni ni kitu gani kiliisibu ndege hiyo.chanzo bbc,(A.I).

Maajabu:Kijana ang'olewa meno 232

Madaktari nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani .

Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.

Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.chanzo bbc,(A.I).

PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA MAKAMPUNI UA SOMITO NA CITI BANK 


PG4A5925
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na   viongozi wa  Citi Bank  ofisini kwake  jijini Dar es salaam Julai 23, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Uchukuzi , Dr. Harrison Mwakyembe. 

PG4A5939
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Citi Bank baada ya kuzungumza nao , Ofisini kwake jijini  Dar es salaam julai 23, 2014. kushoto ni Waziri wa Uchukuzi aliyemabatana na ujumbe huo na kushoto kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary Nagu.

PG4A5978
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa kampuni ya  Sumitomo Chemicals ya Japan wanaokusudia kuwekeza  kiwanda cha mbolea nchini na katika kilimo  cha mpunga. Wapili kushoto  ni Waziri wa  Kilimo , Chakula na  Ushirika, Mhandishi Christopher Chiza.

Ajali ya Ndege:Miili imewasili Uholanzi 

Miili ya abiria wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Eindhoven
Ndege mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa Ukraine , imewasili Uholanzi.
Theluthi mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo yaani 193 ni raia wa Uholanzi na nchi hiyo iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko nusu mlingoti.
Mfalme na malkia wa Uholanzi , waziri mkuu na viongozi wengine wako Eind-hoven pamoja na jamaa za waliouawa kupokea miili ya marehemu.
Bado haijaeleweka ni miili mingapi kati ya ile wa watu 282 waliouawa , imefikishwa hapo jana.(P.T)
Miili ya abiria wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Eindhoven
Vifaa vya kurekodia mienendo ya ndege hiyo vimekabidhiwa wapepelezi wa Uingereza na maelezo kuvihusu yatakabidhiwa majajusi wa uholanzi .
Maafisa wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.
Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.
Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
Chanzo:BBC

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA TATHMINI YA UTEKELEZAJI BRN 

1
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu akichangia hoja wakati wa mkutano wa kupitia taarifa ya mwaka mmoja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN) uliofanyika leo Jumatano Julai 23, 2014 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Bashir Mrindoko

2.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akichangia hoja wakati mkutano wa kupitia taarifa ya mwaka mmoja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano Julai 23, 2014 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Asha- Rose Migiro na (katikati) Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais- Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB), Bw. Omari Issa.

3.

 

Sunday, July 20, 2014

Jinsi mwanamke alivyojipatia mamilioni kutokana na uvutaji sigara wa mumewe

sigarr
Kampuni ya upili kwa ukubwa katika utengenezaji wa sigara nchini Marekani imeagizwa kulipa kitita kikubwa cha dola billioni 23 kwa mke wa mwathiriwa mmoja wa sigara aliyefariki kutokana na saratani ya mapafu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mjane huyo Cynthia Robinson alichukua hatua dhidi ya kampuni ya sigara ya R.J Reynolds baada ya kifo cha mumewe aliyekuwa na miaka 36.
Kampuni hiyo imeyataja malipo hayo kama yasio na haki na kusema kuwa itakata rufaa.
Wakili wa bi Robinson amesema kuwa kampuni hiyo ya sigara iliuza sigara hizo bila kutoa tahadhari yoyote kuhusu tishio la uvutaji wake.

Picha za mechi ya Taifa Stars vs Msumbiji pamoja na stori

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta
akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Msumbiji katika mchezo uliofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji.
Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa katikati ya mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu
akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wa kuwania tiketi ya Fainali za
Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 
 Thomas Ulimwengu  akichuana na beki wa Msumbiji, Josemar Machaisse.
 Huniwezi…Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu
akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior.

 Mshambuliaji wa Stars, Khamis Mcha akiwa katika harakati za kufunga goli.
 Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia balo la pili la 
Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka ‘Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete’.

Walinzi 20 wa mpakani wauawa Misri 

Maafisa nchini Misri wanasema kuwa takriban walinzi 20 wa mpakani wameuawa katika shambulizi la kizuizi kimoja cha ukaguzi magharibi mwa taifa hilo,karibu na mpaka na Libya.
Duru za usalama zinasema kuwa washambuliaji hao walitumia vifaa vya kurusha magurunedi na silaha kali kutekeleza shambulizi hilo.
Chombo cha habari cha taifa hilo kiliwataja watu hao kuwa watu wanaofanya magendo katika eneo hilo la mpaka huku jeshi likisema kuwa walikuwa wanamgambo.
Maafisa wa usalama wanaamini kwamba wanamgambo kutoka Libya wanajaribu kushirikiana na wapiganaji wa Misri ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi yao katika eneo la Sinai tangu kuondolea madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.(Chanzo:BBC)

Saturday, July 19, 2014

GAZA:Israel yaendeleza mashambulizi yake 

Wakimbizi wa Gaza
Maafisa wa Umoja wa mataifa katika eneo la Gaza wanasema kuwa idadi ya raia wa Palestina walioachwa bila makao na ambao kwa sasa wanatafuta makao kufuatia mashambulizi ya nchi kavu yanayotekelezwa na Israel sasa imeongezeka maradufu kutoka elfu ishirini na mbili hadi elfu arobaini.
Raia wengi wameelekea Magharibi mwa Gaza ili kutoroka mashambulizi ya Israel.
Baada ya utulivu siku ya ijumaa kuna ripoti kwamba mizingi ya israel imefanya mashambulizi mengine usiku kucha.
Zaidi ya raia 60 wa Palestina wakiwemo watoto tisa wanadaiwa kuuawa tangu kuanzishwa kwa oparesheni ya nchi kavu na hivyobasi kuongeza idadi ya watu waliouawa kufikia 300.
Jeshi la Israel linasema kuwa mwanajeshi mmoja wa Israel aliuawa siku ya ijumaa kufuatia ufyatulianaji wa risasi wa wenyewe kwa wenyewe.(P.T)

Muda wa majadiliano na Iran waongezwa

Viongozi wajadiliana na kuhusu mpango wa nuklia wa Iran
Wawakilisha wa mataifa sita yenye uwezo mkubwa duniani pamoja na Iran wameongeza kwa miezi mengine minne makubaliano ya mpango wa nuklia wa Iran.
Wajumbe wanaokutana mjini Vienna wamesema kuwa tofauti zilizopo ni kubwa mno kuafikiwa kabla ya kukamilika kwa siku ya mwisho hapo kesho.
Katika taarifa iliosomwa kwa pamoja, afisa, anayesimamia sera za kigeni katika muungano wa Ulaya Catherine Ashton pamoja na waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Javad Zarif wamesema kuwa licha ya hatua muhimu kupigwa kuna tofauti kubwa.
Majadiliano sasa yataendelea hadi Novemba 24. Wakati huo Marekani itatoa takriban dola billioni 3 za Mali ya Iran ili taifa hilo libadilishe utajiri wake wa Uranium kuwa mafuta.
Katika makubaliano ya mda yalioafikiwa mwezi Novemba mwaka uliopita ,Iran ilikubali kusitisha uzalishaji wake wa Uranium kwa lengo la kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa vilivyoigharimu takriban dola bilioni saba.(P.T)

Tamko La Chadema Kuhusu Mchakato Wa Katiba  

1_aa874.jpgMhe.Freeman Mbowe!
"Mchakato wa Katiba ni mchakato wa Kisiasa.
Mchakato ukiharibiwa, hutengeneza Ombwe.
Makundi mbalimbali yamekuwa yakitoa wito ili kuokoa mchakato wa Katiba.
Rai ya kututaka UKAWA kurudi bungeni, bado haijazingatia yale yaliyotufanya tutoke Bungeni.
Viongozi wa UKAWA tumekaa na kujadili kwa kina.

Ni uwendawazimu kurudi bungeni kwa mazingira yale yale.
UKAWA tumechukua nafasi kuziba Ombwe la uongozi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Tuna ushahidi wa namna CCM wanavyopanga kuvuruga mchakato wa Katiba.
Sisi tutapanga namna ya kuandaa Plan B.
Hatuko tayari kwenda kwenye uchaguzi Mkuu mwakani kwa Sheria hizi hizi.

Siku ya Jumapili baada ya vikao hivi, tutatoka na maazimio na tutaongea na vyombo vya Habari.
Tutakaa na kujadili kwa kina kwenye vikao hivi vya leo na kesho, pamoja na agenda nyingine, lakini ni lazima tutoke na maamuzi mazito.

Tunamtaka Rais aache tabia ya ukigeugeu.
Tunamtaka Rais kwa muda mchache aliobakia madarakani, ajifunze hata kwa kujilazimisha, aache tabia ya unafiki".
Mhe.Mbowe ameyasema hayo kwa niaba ya Chama katika hotuba yake fupi ya ufunguzi wa vikao vya Kamati Kuu ya CHADEMA vinavyoendelea hivi sasa katika Ukumbi wa Mbezi Garden Hotel iliyopo Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam.
Mhe.Tundu Antipus Lissu,
Mjumbe Kamati Kuu,
CHADEMA.
18/07/2014.
Ahsanteni sana!!!

Friday, July 18, 2014

Tathmini ya ajali za barabarani kuanzia January mpaka June 2014 hii hapa

 

ajali
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama Barabarani Dcp Mohameed Mpinga katoa tathmini ya ajali za Barabarani kuanzia Mwezi Januaary mpaka June ikiwa n i kipindi cha nusu mwaka na hivi ndivyo hali ilivyo.
mpinga
  TATHIMINI YA MATUKIO YA AJALI ZA
 BARABARAN JAN-JUNE 2013/2014

Takwimu zinaonyesha kuwa juhudi zetu zimefanikiwa kwa kupunguza ajali na majeruhi, ingawa kuna ongezeko la watu waliofarika katika ajali kwa Jan – June 2014.
S/N0
JAN-JUNE 2013 JAN –JUNE 2014 ONG/PUNG (%)
1 IDADI YA AJALI 11,311 8,405 -          2,906     (26%)
2 VIFO 1,739 1,743                  4   (0.2%)
3 MAJERUHI 9,889 7,523 -          2,366     (24%)

Taarifa mpya juu ya ndege nyingine ya Malaysia iliyoanguka Ukraine

malay2
Ndege ya Malaysia iliyokuwa imebeba abiria 295 ndani yake imeanguka Mashariki mwa Ukraine ikitokea Amsterdam kwenda Kuala Lumpur, kufuatia tuhuma kuwa ilitunguliwa.
malay
Miili kadhaa ya watu imesambaa katika eneo ilipoanguka ndege hiyo karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodaiwa kushikiliwa na waasi.
Ndege hiyo ya MH17 ilikuwa inakaribia kuingia katika ardhi ya Urusi wakati ilipopoteza mawasiliano.
malay3
Pande zote mbili serikali ya Ukraine na waasi wamekanusha kuitungua ndege hiyo katika mji ulio karibu na mpaka wa Urusi.

Unamkumbuka Rapa aliyejikata sehemu za siri?kaja na hii mpya

johnson
Mwezi April ilisambaa stori juu ya mwanamuziki wa Hip Hop Andre Johnson kujikata sehemu zake za siri ambapo stori hiyo iliripotiwa na vyombo kadhaa duniani lakini mbali na kujikata sehemu hizo alijirusha kutoka juu ya jumba moja mjini Los Angeles.
Ukubwa wa stori hii umefanya wadau mbalimbali wa vyombo vya habari kutaka kufahamu sababu za yeye kuamua kufanya vitendo hivyo ambavyo pengine vinaashiria hata kuyagharimu maisha yake.
Johnson ametoa sababu zake na kubwa zaidi akisema kuwa yeye ana akili timamu hana matatizo ya akili ingawa aliwahi kutumia dawa za kulevya lakini alikuwa anajifahamu mahojiano hayo ameyafanya kupitia kituo cha televisheni cha E! kilichopo Marekani.
Sababu nyingine aliyoisema kwenye mahojiano hayo amesema kuwa yeye sio Mwandamu>>’Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha matatizo yangu’
‘Suluhu yangu kwa matatizo yangu ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu mini ni mungu vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi.siko hapa duniani kama mwanadamu bali mungu ”
Madaktari walishindwa kuunganisha sehemu hizo za siri za Johnson na kwa sasa anaishi bila sehemu hizo za siri na kusema kuwa anafurahi yuko hai,hilo ndilo jambo muhimu zaidi kwake, hata bila ya uume wake.

Kampuni ya Microsoft inavyojiandaa kupunguza ajira elfu 18 za wafanyakazi wake

microsoftkm
Kampuni ya kiteknolojia ya Microsoft inatarajia kupunguza takribani ajira elfu 18 za wafanyakazi wake na kuweka rekodi ya kupunguza watu wengi zaidi katika historia ya kampuni hiyo kwa miaka 39.
Punguzo kubwa litafanyika kwa ajira elfu 12 kwa kitengo chake cha Nokia ambacho kampuni hiyo ilinunua mwezi Aprili.
Punguzo hilo ni kubwa tofauti na matarajio ya watu 6000 yaliyokuwepo awali.
Kampuni hiyo inaajiri watu laki moja na 27 dunia nzima ikiwa ni pamoja wa wafanyakazi 3,500 nchini Uingereza.
Kampuni hiyo imekataa kusema ni ajira kiasi gani zitapunguzwa nchini Uingereza ikiwa ni matokeo ya mabadiliko hayo

Jinsi mtoto wa miaka sita alivyobakwa shuleni nchini India

bbb
Polisi Kusini mwa India wameandikisha kesi ya ubakaji ambapo inadaiwa kuwa mtoto wa shule mwenye umri wa miaka 6 alibakwa na wafanyakazi wawili wa shule moja maarufu mjini Bangaloer.
Uhalifu huo unadaiwa kutekelezwa wiki mbili zilizopita.
Mtoto huyo alibakwa na mlinzi pamoja na mwalimu, lakini kwa sababu ya kuwepo walinzi wengi katika shule hiyo, polisi bado wanachukua muda kuchunguza mlinzi aliyehusika.
Polisi wanasema kuwa mtoto huyo alibakwa tarehe mbili Julai , lakini wazazi wake waligundua hilo siku chache zilizopita baada ya mtoto huyo kulalamika kuumwa na tumbo na kupelekwa hospitalini.
Wakati huo mamia ya wazazi wameandamana nje ya shule wakivunja milango na kupiga mayowe kulaani tukio hilo.

Kesi ya Mbasha imesomwa tena leo na hiki ndicho kilichoamuliwa na Mahakama

7mbsh
Mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel Mbasha leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili yanayo mkabili ya ubakaji.
Katika kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani tangu kesi hiyo imeanza Mbasha hajapeleka wakili yoyote.
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.
6mbsh
3mbsh

Thursday, July 17, 2014

£8m zamhamisha Demba Ba hadi Uturuki 

demba_fadeb.jpg
Usajili mpya na mikataba mipya kwa wachezaji vinara ndio shughuli kuu inayoendelea sasa kabla msimu mpya wa michuano kuanza.
Pamoja na kasheshe zinazomuandama, Suarez sasa yuko Bacelona 100% baada ya kuihama Liverpool, nae Demba Ba tayari amewasili Uturuki anakotarajiwa kukamilisha uhamiaji wake kutoka Chelsea hadi Besiktas kwa gharama ya £8m.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa mika 29 ameyathibitisha hayo katika mtandao wa Twitter akionekana tayari kavalia jesi ya Besi-ktas. "amesema yaliyobaki ni kukamilisha ukaguzi wa kiafya na kuweka saini mkataba.
Demba Ba amewahi kuifungia Chelsea angalau mabao 14.
Hivyo Chelsea wamejibu kwa kumshawishi Filipe Luis aihame Atletico Madrid ingaje Mbrazil huyo yuko katika safu ya ulinzi.
Msimu uliopita Luis alishiriki mechi zaidi ya 40 na kilele ikawa Atletico kushinda la liga kwa mara ya kwanza tangu 1996 na pia wakafikia fainali ya Champions League.(E.L)

TETESI ZA SOKA ULAYA 

Chelsea wapo tayari kumuuza John Obi Mikel, 27, wakati wanapanga kumnyatia kiungo wa Real Madird Sami Khedira, 27 ambaye pia anatakiwa na Arsenal (Daily Express), Arsenal wanatarajia kuthibitisha siku la Alhamisi usajili wa kiungo wa Newcastle Mathieu Debuchy, 28, kwa pauni milioni 10 (London Evening Standard).
Tottenham watampa beki Jan Vertonghen, 27, mkataba mpya wa miaka mitano, pamoja na kuongeza mshahara hadi pauni 45,000 kwa wiki (Daily Mail), boss mpya wa Manchester United Louis van Gaal anataka kuwaondoa takriban wachezaji kumi wakiwemo Ashley Young, Patrice Evra, Fellaini, Nick Powell, Anderson, Javier Hernandez, Wilfried Zaha, Nani, Tom Cleverly, Chris Smalling na Bebe (Daily Star na Daily Mirror).(P.T)
Mark Hughes wa Stoke City yuko karibu kumchukua winga wa Liverpool Oussama Assaidi, 25 kwa uhamisho wa takriban pauni milioni 7 (Daily Telegraph), meneja wa QPR Harry Redknapp anapanga kumchukua beki wa kati wa Aston Villa Ron Vlaar kwa pauni milioni 4 (Birmingham Mail), Liverpool watapambana na Tottenham kumwania beki wa kushoto wa Swansea Ben Davies (Daily Star).
Toni Kroos anajiandaa kuhamia Real Madrid kwa mkataba wa euro milioni 30 akitokea Bayern Munich (Bild). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. 
Kutoka kwa Salim Kikeke

NELSON MANDELA INTERNATIONAL DAY 

In November 2009, the UN General Assembly declared 18 July as "Nelson Mandela International Day" in recognition of the former South African President's contribution to the culture of peace and freedom. General Assembly resolution A/RES/64/13 recognizes Nelson Mandela's values and his dedication to the service of humanity, in the fields of conflict resolution, race relations, the promotion and protection of human rights, reconciliation, gender equality and the rights of children and other vulnerable groups, as well as the uplifting of poor and underdeveloped communities. It acknowledges his contribution to the struggle for democracy internationally and the promotion of a culture of peace throughout the world.
The UN resolution urges all countries, the UN, civil society, business and Non Governmental Organizations to celebrate this day by dedicating time towards community service. In line with the essence of Nelson Mandela Day, the focus of this event will be on giving the gift of time.
This day is intended to encourage people to dedicate their service to values that will improve our world and support the development of children. We hope you will join us in this commemoration.
This year will be the first to be commemorated after Nelson Mandela lost his life in December last year at the age of 95. The Nelson Mandela International Day is a call to everyone to devote 67 minutes of time to helping others, as a way to mark Nelson Mandela International Day.
For 67 years Nelson Mandela devoted his life to the service of humanity — as a human rights lawyer, a prisoner of conscience, an international peacemaker and the first democratically elected president of a free South Africa.
You are invited to commemorate the 67 minutes through community service at Sinza Special needs school in Kijitonyama area-behind Mabatini police station (off Africa Sana road) in Dar es Salaam. Basically, activities that would be undertaken would involve cutting grass, painting, spending time with the children, cleaning, cooking and supporting the school.
Please feel free to bring any tools or cleaning materials that could assist in performing this community service. Any donations of clothing, spades and hoes, toys, books, meals, would also be welcomed.
Event: Nelson Mandela International Day
Where: Sinza Special needs school Kijitonyama area behind Mabatini police station off Afrika Sana road
When: Friday, 18th July, 2014 from 09:30am – 12:00pm
What: Voluntary community service work
The media advisory has been issued by Stella Vuzo, UN Information Center(UNIC) 0767 100 902.