WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATOA MAAGIZO
Naibu
waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele akitoa maagizo
alipotembelea ofisi za TMAA, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TMAA,
Bw. Paul Masanja.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Stephen
Masele ameiagiza Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kuimarisha
ukaguzi maeneo ya migodini hususan maeneo ya migodi mikubwa.
Mhe.Maselle alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za Wakala zilizopo maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
Alibainisha
kuwa TMAA haina wakaguzi ambao wanakuwa ndani ya mashimo ya migodi hiyo
hivyo kuna umuhimu wa kuwa na mkaguzi mwingine ambaye atakuwa maalumu
kwa ajili ya kufanya ukaguzi ndani ya mashimo.
“Ugakuzi makini utahusika pia na kuhakiki
gharama za uwekezaji na uendeshaji wa migodi mikubwa ya ili kudhibiti
mapato ya Serikali”, alisema Masele na kuongeza kuwa madini
yanayosafirishwa kwa mashine kutoka katika mashimo ni kiasi kidogo
tofauti na yale ambayo yanatolewa kwa kuokotwa kwa mkono kutoka huko
katika mashimo.
Aidha,
Naibu Waziri huyo aliipongeza TMAA kwa kufanikisha kukamatwa kwa
mameneja watatu wa Kampuni ya Aureus Ltd ambao wanatuhumiwa kukwepa kodi
na kutorosha dhahabu nje ya nchi. “TMAA ni jicho la Wizara, mmefanya
ukaguzi na mmebaini haya, endeleeni hivyo hivyo, taarifa zote
mtakazoleta tutazifanyia kazi”, alisisitiza.
Alisema
ukaguzi uliofanywa na TMAA unaonesha uzalishaji wa kampuni hiyo ni
mkubwa kuliko uliokuwepo kabla ya kuanza kwa ukaguzi. “Tukigundua
vitendo vya utoroshaji ama ukwepaji wa kulipa mapato kwa namna yoyote,
tutachukua hatua kali ili iwe ni fundisho kwa wengine wenye tabia za
namna hii” alionya.
Naye
Mtendaji Mkuu wa TMAA, Paul Masanja alisema TMAA itaendelea kufanya
kazi kwa kasi zaidi ili kuendelea kuwabaini wale wote wasiyowaaminifu na
kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake.
“Tunakuahidi
Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba sisi hatutorudi nyuma, tutaendelea kutoa
ushirikiano wa karibu zaidi na tutafanya kazi zetu kwa ufanisi ili
kufikia malengo” aliongeza.
No comments:
Post a Comment