WAUWAJI WA BALOZI WAKAMATWA LIBYA
Mkuu
 wa bunge la Libya anasema kuwa watu kama 50 wamekamatwa kwa kuhusika na
 mauaji ya balozi wa Marekani mjini Benghazi juma lilopita.Mohammed 
Megaryef, kiongozi wa bunge, alisema hakuna shaka kuwa shambulio hilo 
lilikuwa limepangwa na siyo tu la kulipiza kisasi kwa filamu ya Marekani
 iliyokejeli Uislamu.
Akizungumza na shirika la habari la Canada, CBS, Bwana Megaryef alisema anaamini wageni wenye uhusiano na Al-Qaeda walihusika.
Balozi
 wa Marekani, Chris Stevens, na Wamarekani wengine watatu, waliuwawa 
wakati guruneti lilipopiga ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi na 
kuwaka moto.
 Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

No comments:
Post a Comment