TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, September 10, 2012

USAFIRI WA TRENI DAR ES SALAAM WAANZA KWA MAJARIBIO









Usafiri wa treni jijini Dar es salaam utaanza rasmi mwezi Oktoba baada ya kukamilika kwa maboresho ya reli kutoka Ubungo hadi stesheni.

Akizungumza jana baada ya kufanya safari ya majaribio Naibu waziri wa Dk Charles Tizeba alisema kufikia mwezi ujao treni itaanza kubeba abiria ili kupunguza matatizo ya usafiri kwa wakazi waishio maeneo inapopita treni hiyo.
“Kufika Oktoba tutakuwa tumeanza kutoa huduma maana leo tumeanagalia uwezekano na tumeona tunaweza ufanya huduma na kurekebisha kasoro zilizobaki” alisema Dk Tizeba .

Dk Tizeba alisema kuwa reli hiyo kwa sasa bado haijakaa vizuri hivyo inahitaji kurekebishwa ili treni hiyo iweze kwenda kasi zaidi na kubomolewa kwa nyumba zilizojengwa jirani na reli hiyo.

“Inashangaza sana kwani kuna watu wamejenga nyumba zao jirani kabisa na reli na wengine wamediliki kujenga mita moja kutoka relini, hii inahatarisha maisha yao wenyewe na hata wasafiri watakaotumia treni”

Hivyo alisema kuwa tayari watu hao wametaarifiwa juu ya kuondoka katika maeneo hayo na kwamba watatakiwa kuvunja wenyewe na wakikaidi basi watavunjiwa ili huduma hiyo ianze kutolewa.

No comments:

Post a Comment