TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, September 17, 2012

MSAFARA WA NYUMBU SERENGETI
WATALII WAFURIKA SERENGETI KUSHUHUDIA MSAFARA WA NYUMBU UKIREJEA NYUMBANI HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI WAKITOKEA MAPUMZIKO
Msafara maarufu duniani unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu umeanza kurejea katika makazi yao ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakitokea mapumziko katika nchi ya jirani.
Kila mwaka, nyumbu pamoja na wanyama wengine kama pundamilia na swala hufanya mzunguko maalum unaochukua miezi 12 ya mwaka ambapo miezi kumi kati ya hiyo huwepo nchini katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na iliyobaki hutumiwa na wanyama hao katika eneo la Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.
Mwaka huu msafara huu unaohusisha wanyama zaidi ya Milioni Moja na Nusu na ambao hutembea katika mzunguko wa takribani Kilometa 1,000 umewahi sana kurejea nchini ukitokea mapumziko nahii kwa mujibu wa taarifa za kitaalamu inatokana na kuwahi kunyesha kwa mvua katika eneo la Serengeti ambapo imesababisha kuwepo na nyasi nzuri ambazo ni chakula muhimu kwa wanayama hawa.
Changamoto kubwa wanayokutana nayo msafara huu mara unaporejea nyumbani ni tukio la kuvuka Mto Mara ambao umejaa wanyama wakali aina ya mamba na viboko ambao nao huwa ni msimu wao wa kujipatia chakula kwa kuvizia na hatimaye kuwakamata wanyama hawa mara wanapovuka mto.
Watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakifurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushuhudia tukio hili adimu la kuvuka Mto Mara ambalo wengi wao wamekuwa wakiliona kupitia filamu mbalimbali zilizotengenezwa katika eneo hili.

No comments:

Post a Comment