Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imesema hakuna mtu aliyefariki kutokana na vurugu
siku ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu uliofanyika Jumapili
iliyopita kama ililivyodaiwa na gazeti moja linalotolewa kila wiki hapa
nchini.
Kwa
mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar na
kutiwa saini na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed imeeleza hadi sasa hakuna taarifa
yoyote ya kifo kilicho sababbishwa na vurugu hilo iliyoripotiwa.
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kujeruhiwa
watu kutokana na vurugu za baadhi ya vikundi vya wananchi
vilivyojipanga kuwazuia wananchi wengine kwa makusudi kushiriki katika
zoezi la kupiga kura.
Kuhusu
tuhuma zilizo tolewa dhidi ya Makamo wa Pili wa Rais katika zoezi la
upigaji kura taarifa hiyo ilieleza kuwa maelezo hayo siyo ya kweli na
kwamba zinalenga kumchafulia jina Kiongozi huyo wa ngazi za juu
Kufuatia tuhuma hizo Serikali imemtaka Mhariri wa Gazeti la FAHAMU kuthibitisha kwa maandishi tuhuma walizoandika dhidi ya Mheshimiwa Makamo wa Pili wa Rais au kumuomba radhi kwa maandishi kupitia Gazeti lake la FAHAMU katika kipindi kisichozidi siku saba(7) kuanzia tarehe ya taarifa hii. Vyenginevyo Serikali itachukuwa hatua zinazofaa dhidi ya wahisika wote.
Aidha
taarifa hiyo imeeleza kusikitishwa kwake na taarifa zilizotolewa na
kiongozi mmoja wa Ngazi za juu wa CUF kupitia gazeti hilo kwa kumtaja
Makamo wa Pili wa Rais kuwa kiongozi wa juu wa serikali ya Umoja wa
Kitaifa Zanzibar aliyejitosa kuharibu matokeo ya kura kwa kuingia katika
baadhi ya vituo kama kiongozi wa Wawananchi.
Tuhuma hizo si za kweli na zisingepaswa kutolewa na Kiongozi wa juu wa chama cha siasa kwani kiongozi huyo anaelewa fika kwamba tuhuma hizo zinachafua jina la kiongozi huyo na kuhatarisha Umoja wa Taifa Letu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 19/09/2012.
No comments:
Post a Comment